Thursday, 28 September 2017

MTANDAO WA WATSAPP WAVURUGWA NCHINI CHINA NA SERIKALI


Huduma ya mtandao ya WhatsApp imeharibiwa nchini China wakati ambapo serikali inaimarisha usalama kabla ya kufanyika kwa mkutano wa chama cha Kikomyunisti mwezi ujao.
Watumiaji wake wamekumbwa na tatizo katika utumizi wa mtandao huo kwa zaidi ya wiki moja huku huduma ikikosekana.
Wakati mwengine, huduma hiyo imezimwa na ilikuwa inaweza kupatikana kupitia mtandao wa kibinafsi wa VPN ambao unasimamia mitandao ya China pekee.
WhatsApp ni huduma ya facebook ya pekee inayoruhusiwa kurusha huduma zake nchini China.
Facebook ndio huduma kubwa ya mtandao huku programu ya picha ya Instagram ikiwa pia haipatikani.
Mwandishi wa BBC nchini China anasema kuwa huduma ya WhatsApp ilianza kutopatikana mtandaoni zaidi ya wiki moja iliopita.
Vipimo vya huduma zake siku ya Jumanne vilionyesha kuwa watumizi wa China hawakuweza kutuma video ama hata picha kwa watu wengine nje ya China.
Uharibifu huo unafuatia masharti ya simu za Video na picha mnamo mwezi Julai, ambayo baadaye yaliondolewa

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search