Friday, 29 September 2017

NATAKA KUZAA-EPISODE YA SABA


MTUNZI: JENNIFER ALPHONCE
SIMU: 0683777152
SEHEMU YA SABA
Mambo yalikuwa yakitokea harakaharaka kiasi kwamba sikuweza hata kunyanyua mdomo, nilibaki tu nikiwa nimetoa macho.
Melania aliendelea kupayuka, “mwizii….. Mwizi…..”
Watu walifika na kumvuta Shati Frank, nilishangaa vitu vyetu vimefikaje kwenye mikono ya Frank.
Wakati nikiwa bado sielewi nini kimetokea ghafla alitokea Innocent alipangua watu waliokuwa wamemshika Frank na kisha akamvutia mikononi mwake.
“Nini…. Kuna nini?” Aliwauliza.
“Huyu jamaa ameiba vitu vya watu.” Akamgeukia Frank na kumtazama.
“Mna uhakika kwamba ameiba?”
“Ndiyo si hivyo hapo kavishika mkononi.”
Wakati sisi tukitokea madarasani kwetu kwa ajili ya kuelekea Shuttle Point kupanda gari Frank alikuwa akija mbele yetu huku akiwa ameshikilia wallet yangu na simu ya Melania.
“Mna uhakika na wewe unamuitia mwizi mtu kabla hujamuuliza.” Innocent aliendelea kufoka.
Melania alinyamaza, tulishindwa cha kuongea tukabaki tukitazamana.
Na wale watu waliokuwa tayari wameshamshika Frank na kutaka kumpiga walibaki wameduwaa.
“Mmemsikiliza alichowaambia hivi unafikiria angekuwa ameiba angekuwa amevishikilia tu hivi anatembeatembea navyo.” Innocent aliongea hakuna aliyejibu.
“Kwani amevipaje vitu vyetu.” Niliweza kuuliza.
“Waambie Frank.” Alisema.
Alishikwa na kigugumizi Frank, nilishangaa Frank huyu mwenye kuweza kuongea ameshikwaje na kigugumizi. Mwishowe aliweza kuongea.
“Sociolah siku ile wakati ulivyokaa pale mbele halafu ukanyanyuka kwa hasira na kuelekea nyuma ulidodosha wallet yako.” Nilishangaa sana wala sikuwahi kuhisi kama ningeweza kuwa nimedondosha wallet yangu pale.
“Jioni ya siku ile nilikufata pale mgahawani ili nikukabithi wallet yako lakini mlinitukana na kisha mkaondoka kabla sijakukabithi wallet yako na baada ya hapo mliondoka wote Melania alisahahu simu yake pale mezani, nilichukua siku ile na nikaja pale mgahawani na nikataka kuwakabidhi mkanimwagia juisi.”
Kwa kweli ilikuwa ni aibu kubwa sana mbele za watu kila mtu alitutazama kwa jicho kali tulishindwa kunyanyua sura zetu.
“Nimeamua kuwakabidhi kwa maana kila wakati nikitaka kuwakabidhi huwa hamtaki. Bahati mbaya simu ya Melania ilizima mda mrefu tu, nikaichaji kwa chaja ya mwenzangu kule chumbani lakini wala mimi sijui kuifungua simu yake, ningeweza kuwajulisha kwamba simu ninayo lakini ilishindikana.” Nilishindwa cha kuongea kwa kweli ilikuwa ni aibu sana nilitazama kando.
“Wallet yako hii hapa hakikisha kama iko salama na Melania simu yako hii hapa iangalie pia.”
Aliipokea kwa fujo na papara zote aliikagua simu yake ilikuwa kama ilivyokuwa cha zaidi alikuwa ameichaji. Aliifungua na kukuta kila kitu kiko salama wala havikufunguliwa, kwa kweli nilishindwa hata kufungua wallet yangu.
“Fungua Sociolah uangalie.” Nilifungua, nilikuta fedha taslimu shilingi laki tano kama zilivyokuwa kila kitu changu kilikuwepo na hakuna kitu kilichopunguka wala kuongezeka, nilishangaa sana.
Melania alishindwa hata kumshukuru Frank alihisi aibu aliondoka ghafla huku akilia na kukimbilia kwenye gari.
Watu waliokuwepo wameanza kukusanyika pale walianza kuondoka na mwishowe tulibaki mimi, Frank na Innocent.
Innocent alinitazama tu nilinyanyua uso na kuwakuta wamesimama mbele yangu kana kwamba hawana mahali pa kwenda.
“Ahsante Frank, and am sorry for everything.” Niliweza kusema.
“Usijali.” Alivyomaliza kusema aliondoka.
Innocent alibaki akinitazama tu.
“Kuwa makini.” Aliongea na kisha kuondoka.
Niliwaangalia hadi walipoishilia kwa aibu nilitoka pale na kuingia kwenye gari sikutaka hata kwenda kukaa karibu na Melania. Gari lilipojaa dereva alikuja na tulianza safari ya kuelekea Mabibo.
Tulipofika Mabibo habari ile ilikuwa gumzo katika kikundi chetu cha WhatsApp.
“Kumbe jamaa alikuwa mwizi duuh!” Mtu mmoja aliongea.
“Hamna wewe hukuona vizuri wala hukusikia mchezo mzima ulivyokuwa wamemsingizia tu, CR umemsingizia mtoto wa watu kaiba jamani.”
“Sio mimi.” Nilijitetea.
“Ni Melania.”
“Aah na wewe si mlikuwa naye bana mnanyanyasa sana mtoto wa watu.” Aliongea
“Ila kajamaa kanaweza kuwa kaizi hadi mkopo apate tutakuwa tumepigika vibaya, hivi hayupo humu.”
Mdada aliingia, “hana simu ya WhatsApp.”
“Msijali boom litaingia hivi karibuni na atanunua simu yake.” Innocent aliandika.
“Halafu jamaa acheni dharau za ajabu ajabu mimi kitendo kilichotekea leo sijakipenda, sio leo tu nawaona jinsi mnavyomchukulia Frank.” Innocent alikuja juu.
“Ni sawa Frank ametokea kwenye Familia ya kimasikini lakini jamaa anajua ni nini kimemleta hapa, subirini tu mwenzenu anaishi maisha ya shida subirini hata apate basi boom lake aweze kununua simu sio vizuri kumsema mtu kulingana na sehemu tulizopo wengine hapa wana maisha magumu kwao lakini bado wanaigiza bora Frank anaishi maisha yake halisia.” Aliongea kiukweli maneno yake yalinigusa.
“Amepata mkopo?” Niliuliza.
“Ndiyo amepata na wameshasaini boom wanasubiri tu liingizwe.”
“Sawa.” Nilijibu.
Muda ulienda na tulianza mitihani yetu ya kwanza ubize uliongezeka kati yetu na matukio ya ajabu ajabu hayakuwepo na ilikuwa kwa nadra sana kukutana na Frank aidha darasani au kwenye korido za darasa zetu. Mara nyingi tulikuwa tuko bize sana.
Niliweza kuona Frank akiwa na simu mpya aina ya Tecno Y3+, nafikiri aliinunua baada ya kupata boom lake hata mavazi yake pia yalianza kubadilika kidogo ingawa bado alikuwa akivaa kiushamba ushamba lakini alikuwa na afadhali sio kama hapo mwanzo.
Siku zilisogea na hatimaye sikukuu za Christmas na mwaka mpya zilikaribia, hapo tuliweza kufunga kwa muda wa wiki mmoja na nusu. Baada ya kufunga nilirudi nyumbani.
Ilikuwa ni siku ya ijumaa ambapo Christmas ilikuwa ni jumatatu nilikuwa tu nyumbani sina cha kufanya niliamua kuvuta madaftari yangu na kuanza kupitia pitia kuna sehemu ilinishinda, niliamua kuuliza kwenye kikundi cha WhatsApp hakuna aliyeweza kunisaidia.
Nilikuwa nikihitaji sana kujua hiko kitu lakini hakuna mtu aliyeweza kunijibu.
“Jamani naombeni basi mnijibu.”
Wengine walicheka na wengine waliondoka kabisa hewani.
Nikaamua kutoka hewani na kukaa nilishindwa kuendelea kusoma kwa maana kilikuwa ni kitu cha muhimu sana baada ya muda niliamua kurejea hewani nilishangaa nilishangazwa kukutana na jibu kutoka kwa Frank, alielezea vizuri kiasi kwamba nilielewa.
“Ahsante sana Franklin.” Niliongea.
“Usijali.” Alisema.
Niliona haitoshi nikaamua kuingia sehemu yake ya ujumbe mfupi,
“Thank Frank.”
“Usijali Sociolah.” Alijibu kwa ufupi.
“Well... Unaonekana uko makini sana darasani.” Niliamua kuendeleza maongezi yetu.
“Aah Sociolah si nilishakuambia.”
“Yes I appreciate you.”
“Do you appreciate me.”
“Yes I do.”
“Thank you.”
“Well.”
INAENDELEA….

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search