Thursday, 7 September 2017

SIKILIZA LIVE RAIS AKIKABIDHIWA RIPOTI YA ALMASI YA TANZANITE IKULU

Baada ya jana kamati mbili za bunge kukabidhi ripoti mbili za makinikia ya almasi na biashara ya Tanzanite kwa spika kisha yeye kumkabidhi waziri mkuu, leo zinafika mezani kwa Rais Ikulu. Waziri mkuu, Kassim Majaliwa jana alisema pamoja na uwezo alionao wa kuchukua hatua, anaheshimu sheria na kumpelekea mkuu wa nchi ili wachukue hatua.

Ripoti imesheheni majina mengi kwenye siasa za Tanzania baadhi wakiwa bado kwenye nyadhfa mbalimbali kwenye serikali ilhali wengine ni msumari wao wa pili baada ya ripoti za mwanzo kuwatuhumu. Fuatana nami kutoka Magogoni kujua yatakayojiri.=======

Mh Dotto, mwenyekiti wa kamati ya Tanzanite
=>Mh rais nimshukuru pia mh spika kwani hakutuingilia katika mchakato wa kufanya kazi hii.

=>Niwashukuru pia wajumbe wa kamati yangu

=>Tulipitia Jumla nyaraka 150 kutoka taasisi za serikali na taasisi binafsi.

=>Mkataba wa STAMICO wa almasi ni wa kinyonyaji na hauna tiaja kwa nchi. Tumependeza mkataba huo uvunjwe.

=>Ajira india zaidi ya watu 500,000

=>Tunaomba mfumo wa uthibiti wa madini ya Tanzania uangaliwe

=>Tuwe na sheria maalumu inayosimamia mfumo na uthibit wa uchimbaji wa madini haya haya

=>Tuliangalia mkanda wa video unaoonyesha wizi wa madini ya Tanzania wakishirikiana na watanzania.

=>Mh rais umeamua kuonyesha mfano wa kusonga mbele na kutogeuka jiwe.

=>Mh rais nashukuru kwa kibali chako naomba nikomee hapa

Sasa ni zamu ya Musa Azani Zungu mwenyekiti wa Bunge
=>Mh rais tunakushukuru sana kwa jinsi ulivoanza vita hii. Nakushukuru kwa jitihada zako zate pamoja na waziri mkuu na spika wa bunge.

=>Mita tisini tuu mh rais huu mgodi umetema almasi za kutosha.

=>Kuna jiwe moja liliuzwa dola milioni 2

=>Kamati hii imeundwa na vyama vyote, vyama vyote bila kujali itikadi zao
Musa, Ndasa, Nakasaka, Swale, Taska, Kyula, Rashidi, Ngwali, Shali, Silinde

=>Tuliongozwa na katibu wa bunge Dr Tomas Kashilila.

=>Mikataba imetoka nje na imekuja tuu kusainiwa tuu hapa. Mgodi siyo mapapai useme yanaoza.

=>Kamati imeenda Shinyanga imekuta madhaifu mengi katika usimamizi wa madini, na tulirudi wiki moja baadae tukakuta madhaifu yaleyale.

=>Wajumbe wa bodi toka uchimbaji uanze wametuangusha.

=>Tumegundua mitambo inayowekwa kwenye migodi siyo mipya ila imeandikwa ni mipya ili kuongeza gharama na kukwepa kodi.

=>Mh rais kamati ilifikia wakati na kuona uchungu,

=>Tumekuta kiasi ch tani milioni 105 ambayo yalichimbwa ile michanga inarudishwa tena kwenye mitambo na inatema almasi.

=>Kuna akaunt ya wizara inayopokea maduhuli kutoka shinyanga, ifanyiwe uhakiki. Fedha zilizoingia pale hatujui zimeenda wapi.

=>Kuna akaunti nyingine ipo Uingereza ambayo imefungwa.

=>Tunajiuliza katibu alisainije mkataba wa kuiweka mgodi rehani.

=>Mtanzania aliyekabidhiwa control room hana funguo za kuingia sehemu yenye madini yenyewe.

=>Lipo tatizo la wachimbaji wadogo.

=>Almas haiwezi kupungua uzito wake kwa gesi, tumepoteza 2.4 million dollors kwa almasi kupungua uzito.

=>Wataalam wengine wenye uwezo hawana nia ya kutoa msaada.

=>Mkataba huu hauvumiliki, tuuombe huo mgodi na tuuendeshe hakuna gharama kubwa za kuendesha mkataba wa almasi.

=>Tuupitie huu mkataba na kuona namna kuondoa tatizo hili.

=>Mengi tumeyasema kwenye ripoti yetu na tunaamini yatafanyiwa kazi na kuona hayajirudii. Ipo haja ya hata mikataba mingine kupitiwa upya.

=>Tunakushukuru sana na kukupongeza kwa vita hii

=>Mungu akubariki, Mungu ibariki Tanzania


Mh spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
=>Ndugu zangu watanzania tunapaswa kumshukuru sana Mungu kwa kutupatia rais huyu.

=>Tunafahamu jinsi waafrika tulivyoneemeshwa na mwenyezi Mungu kwa kupewa rasilimali nyingi lakini tuna

=>Baadhi ya sheria zetu zinahitaji kuwekwa vizuri. Mh rais serikali mtakapotuletea sheria ambazo zitahitaji marekebisho tutazifanyia kazi kwa haraka.

=>Hili shirika la STAMICO. Lazima tuwe na chombo cha kitaifa. Ni jukumu la wizara kuiangalia STAMICO upya na kuifanyia marekebisho.

=>Bodi zote zina mfumo wa uendeshaji ambao ni bussiness as usual. Wanakuwa na vikao vinne kwa mwaka, wanaletewa makabrasha na kuyasaini harakaharaka.

=>Bodi zinabadilike na ziende field kuangalia kinachoendelea.

=>Viongozi wote tuliopewa mamlaka tumsaidie mh rais.

=>Viongozi wanasiasa hasa wabunge waliotajwatajwa.

=>Tufike mahali tuwaandikie vyama vya siasa ili vijue watatuletea watu wa aina gani.

=>Tumeamua kummuunga mkono mh rais, lazima watanzania tuanze kufaidika na rasilimali zetu.

Mh waziri wa JMT, Kasim Majaliwa Majaliwa

=>Kamati hizi mbili zimefanya kazi kubwa na kamati hizi zimetokana jitihada zako mh rais.

=>Mimi ningeweza kushughulikia na kuwaita mawaziri na kumpangia kila mtu majukumu yake

=>Kwa kuwa mh rais umeamua suala hili liwe la kizalendo na wazi kwa kila mtanzania na ndiyo maana nikaamua kukuletea ulishughulikie suala hili.

=>Kwa niaba yako na niaba ya serikali, natumia nafasi hii kumshukuru spika na wabunge kwa namna walivolishughulikia suala hili.

=>Ndugu watanznai, Tanzania ni yetu, lazima tushikamane pamoja tuijenge nchi yetu. Lazima tushikamane ili rasilimali zetu zitunufaishe watanzania.

=>Kamati imeonyesha udhaifu mkubwa wa usimamizi wa madini.

=>Watanzania wale waliona hawahudumiwi, sasa lazima waone wanahudumiwa.

=>Mh rais tunajua unazo njia nyingi sana za kupata taarifa. Na sisi ndio njia mojawapo ya kukusaidia kupata taarifa. Sina mashaka na wewe kwamba taarifa hii itakupa faraja.

=>Nisingeomba kuongea mengi maana wananchi wana hamu ya kuona ripoti hii inakabidhiwa na hatua stahiki zinachukuliwa.

=>Mh rais sasa nipo tayari kukukabidhi ripoti hii ya kamati ili kuweza kuona hatua stahiki zinachukuliwa.

Kamati ya almasi imeanza kukabidhiwa, ikifuatiwa na kamati ya Tanzanite


Rais wa JMT anaanza kuhutubia.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search