Monday, 18 September 2017

SIMBA YASHINDA GOLI 3-0 HUKU OKWI AKIENDELEA KUCHEKA NA NYAVU

Mshambuliaji mwenye asili ya Kiganda, Emmanuel Okwi amefunguka na kudai kwa sasa hatazamii kucheza ili kupata kiatu cha dhahabu baada ya ligi kuisha bali malengo yake ni kuisaidia timu yake yake ya Simba SC kupata ushindi.

Okwi amefunguka hayo baada ya kutoka kwenye mchezo wa uliomalizika leo jioni kwenye uwanja wa Uhuru Dar es salaam kwa klabu yake kuichapa Mwadui FC ya Shinyanga mabao 3 -0 na kupata nafasi ya kurejea nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu bara.

"Nawashukuru wacheaji wenzangu kwa ushirikiano na hivi sasa siangalii kupata kiatu cha dhahabu bali kuisaidi timu yangu kupata ushindi, lakini ikitokea kuwa nimepata nitashukuru".

Mabao ya Emmanuel Okwi dakika ya 7 na 67 yaliipa Simba uongozi kabla ya John Bocco kuhitimisha ushindi huo wa pili kwa Simba msimu huu kwa bao safi dakika ya 72.

Simba sasa imefikisha alama 7 ikiwa katika nafasi ya pili nyuma ya Mtibwa Sugar yenye alama 9. Mshambuliaji Emamanuel Okwi amefikisha mabao 8 katika michezo yake miwiwli aliyocheza huku John Bocco naye akifungua akaunti ya mabao ndani ya Simba.

Katika mchezo mwingine jioni ya leo Mbeya City wakiwa nyumbani Sokoine Mbeya wameifunga Njombe Mji bao 1-0

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search