Tuesday, 12 September 2017

WATU WASIOJULIKANA WAMEMPIGA RISASI MEJA GENARAL MSTAAFU -RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) wakioneshwa na  Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe Brigedia risasi  zilizotolewa kwenye mwili wa  Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba  baada ya jana kushambuliwa wakati akiingia  nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo-Picha na IKULU

****

Ikiwa ni siku tano tu zimepita tangu Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Area D, Dodoma, tukio lingine kama hilo limetokea Dar es Salaam ambapo watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wamemshambulia kwa risasi Meja Jenerali Vincent Mritaba.Tukio hilo limetokea jioni ya September 11, 2017 wakati Meja Jenerali Mritaba akiwa anaingia getini nyumbani kwake Tegeta ambapo alivamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa risasi tumboni, begani na mguuni.


Hadi usiku wa jana Madaktari walikuwa wanaendelea na upasuaji kutoa risasi tatu tumboni na kushughulikia majeraha mengine.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search