Saturday, 7 October 2017

Aslay Atamba 'Trending 'You Tube Aishusha Hallelujah ya Diamond

Aslay Atamba You Tube  Aishusha Hallelujah ya Diamond

Ikiwa siku moja imepita toka meneja wa msanii Aslay, Mx kutoa taarifa kuwa ngoma ya ‘Natamba’ imeripotiwa kushushwa katika mtandao wa YouTube hatimaye ngoma hiyo ilirejea hapo jana jioni na kushika namba mbili kama ilivyokuwa awali na hivi sasa imeshika nafasi ya kwanza katika trending ya YouTube.

Hii ni good news kwa mashabiki wa Aslay kwani ngoma hiyo imefanikiwa kushika namba moja katika mtandao wa YouTube kwa kuishusha ngoma ya Diamond Platnumz ft Morgan Heritage ‘Hallelujah’, iliyokuwa imeshika namba moja kwa takribani siku tano mfululizo.

‘Natamba’ ni ngoma nyingine kutoka kwa msanii huyo baada ya kuongeza meneja wake na ina watazamaji 446,213 mpaka sasa.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search