Tuesday, 17 October 2017

BAADA YA KUIBEBA SIMBA KWENYE MCHI DHIDI YA MTIBWA -OKWI ANENA YAFUATAYO

Baada ya kuiwezesha timu yake ya Simba kupata pointi moja kwa bao lake la kusawazisha dakika za majeruhi, mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amezungumza kuhusu matokeo hayo.
Simba ilipata sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru, jana Jumapili ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom ambapo sasa timu hizo zimeendelea kulingana pointi, zote zikiwa na pointi 12 baada ya kucheza michezo 6.
Okwi amesema kuwa katika mchezo huo hawakucheza vizuri na hali kama hiyo huwa inatokea lakini muhimu ni kutoruhusu kupoteza mchezo huo.
“Ni kweli hatukucheza vizuri, huwezi kucheza vizuri siku zote, kuna siku mambo hayaendi sawa lakini tunashukuru kupata pointi moja, mchezo ulikuwa mzuri na hata Mtibwa wenyewe ni wazuri, wana timu yenye kikosi kizuri na ni wazoefu katika ligi,” alisema Okwi baada ya mchezo huo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search