Thursday, 19 October 2017

BARICK WAKUBALI KULIPA SH BILION 700 NA KUINGIA UBIA NA SERIKALI WA 50/50Mwenyekiti wa Barrick Gold anaongea

Anasema Mbele bado kuna matumaini makubwa na wana kazi kubwa ya kufanya na maamuzi yote yanatakiwa yapitishwe na bodi ya wakurugenzi iliyopo Uingereza ambao wanamiliki 64% ya Acacia

Mwenyekiti wa Barrick Gold John L. Thornton amesema kulikuwa na kutokukubaliana kati ya Tanzania na kampuni ya Acacia kuhusu masualaya kodi, hata hivyo wamekubali kulipa dola milioni 300 kwa ajili ya kukuza uaminifu

Kutokana na ugumu wa suala lenyewe wamekubaliana kuunda timu ndogo ambayo itashirikisha pande zote mbili kwa ajili ya kuendelea kushughulikia masuala machache yaliyobakia

Michakato yote itaenda kwa misingi ya uwaziili tuweze kuelewa masuala yote kwa uwazi zaidi

Nampenda kumshukuru rais Magufuli kwa kuwa ndio muanzilishi wa mchakato huu na mfumo huu wa biashara ambao utakuwa ni mfano wa kuigwa duniani, nawashukuru sana....amemaliza

Hotuba ya Mwenyekiti wa Barrick Gold John L. ThorntonProfesa Kabudi anaongea

Nawashukuru Rais Magufuli kwa kuchukua hatua za dhati kuhakikisha madini ya watanzania yanawanufaisha wananchi wake,katika kufanikisha hilo uliunda kamati mbalimbali baada ya kujiridhisha kuwa nchi hii rasilimali zake zinaporwa

Uliunda Kamati ya Prof. Mruma na kisha baadae kuunda kamati ya Prof. Osoro, haya yalimfanya Prof. Thorton kuja kukuona hapa
Baadae uliunda tume nyingine na mimi nikiwa ndio naiongoza , tulianza tarehe 31 Julai na kuihitimisha leo tarehe 19 Oktoba na kutia sahihi tamko la maelewano

Mazungumzo haya hayakuwa mepesi hata kidogo, na kuna wakati yalituteteresha sana ila tukafikia makubaliano

Mapendekezo ya serikali katika majadiliano yalikuwa haya

1. kuainisha fidia kutokana na makosa yaliyofanya na kampuni tanzu ya Barrick hapa nchini

2.Kujadili na kuweka mfumo mpya wa uendeshaji na uchimbaji wa madini ili kuleta mgao sawa kwa makampuni ya madini na serikali

3.Kujadili na kukubaliana muundo na mfumowa uendeshaji utakaowezesha Tanzania kupata manufaa zaidi kutokana na uwekezaji unaofanywa kwenye migodi

4 Kubadilisha mikataba ya uendeshaji ya migodi MDA's ili iendane na marekebisho ya sheria ya madini

5 kuhakikisha wananchi wa Tanzania na jamii inayozunguka migodi wanapata faida kutokana na migodi iliyopo katika maeneo yao

Baada ya mazungumzo haya tulikubaliana muelekeo uwe ufuatao

1. Wamekubali masharti yote yaliyopo katika sheria mpya ya madini zilizotungwa na bunge letu na watahakikisha masharti hayo yanaingia kwenye mfumo wa fedha ambao tumekubaliana

2. Wamekubali serikali itapata hisa katika migodi hiyo kwa asilimia 16 kama sheria ilivyotamka, lakini pamoja na kumiliki migodi hiyo kwa asilimia 16 kwenye mgao itakuwa nusu kwa nusu

3 Migodi hiyo itaweka fedha zinazotokana na madini katika akaunti zilizopo hapa nchini

5. Ofisi zao za London na ofisi zao za Johansburg katika siku za usoni zitahamishiwa Tanzania na makao makuu ya kampuni hiyoyawe Mwanza ingawa wanaweza kuwa na ofisi nyingine sehemu nyingine

6. Kuanzishakampuni nyingine ya kusimamia na kuendesha migodi na makao makuu yake yatakuwa Mwanza na itaongozwa na mtendaji Mkuu,mkurugenzi wa fedha na mkurigenzi wa manunuzi kutoka Tanzania, na ingawa serikali itakuwa na silimia 16 na mgao wa 50/50 wamekubali serikali itakuwa na wawakilishi katika bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo katika kila mgodi

7. Sehemu kubwa ya kazi zitolewazo mgodini sasa kwa kiasi kikubwa inavyowezekana zitafanywa na kampuni za kitanzania na watanzania

8. Kuimarisha huduma za jamii katika maeneo yaliyo karibu na migodi

9. Kila kampuni inayoendesha mgodi kuhakikisha inaachana na utaratibu wakutumia wafanyakazi wa mikataba na badala yake kuajiri wafanyakazi wa kudumu ambao ni wazawa na hawatakaa katika makambi ila kwenye makazi na familia zao, na watajenga barabara ili wafanyakazi waweze kutoka kazini na kwenda makwao

10. Kuajiri watanzania katika nafasi muhimu na za utaalamu, moja kwa moja au kuwafundisha ili baadae waweze kujaza nafasi za uongozi

11. Kutenga bajeti maalumu kwa ajili ya kuchangia utafiti wa kuendesha utafiti wa kuanzisha kiwanda cha kuchakata makinikia na kujenga maabara kubwa ya kupima makinikia

12. Serikali itakuwa na umiliki wa madini yote (rare metals) kama zitapatikana, wao watabaki na dhahabu, shaba na fedha, mafanikio haya sio madogo hata kidogo

13. Kesi zote na mashauri yote yatafanyika hapa Tanzania na sio nje kama ilivyokuwa zamani

14. Suala la fidia lilikuwa suala gumu sana na ndilo lililochukua muda mrefu lazima tupitie nyaraka, ila wamekubali kutoa dola milioni 300 wakati mazungumzo ya jambo hilo yanaendela. Watanzania tuna kila sababu ya kumshukuru Rais Magufuli kwa azma ya kusimamia mambo haya kidete na kwa nguvu zote na kututia moyo na kutuamini sisi badala ya kuleta wataalamu kutoka nje.

50/50 Barrick waliyokubali ni hatua kubwa na mazungumzo yaliyosalia tutafikia muafaka

Prof. Kabudi amemaliza kuzungumza, sasa anazungumza Rais Magufuli

Hotuba ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba KabudiRais Magufuli anasema;
"Kwa mara ya kwanza tangu dunia iundwe tumekubaliana kugawana 50/50 ya faida"

"Naipongeza kamati hii kwa kazi kubwa waliyoifanya kufikia makubaliano haya"

''Tunampongeza ndugu yetu Prof. John kwa kuamua kutuma timu yake kwa ajili ya kuja kufanya mazungumzo"

"Pia wamekubali kulipa kile kinachostahili kwenye Halmashauri"

"Kamati iendelee kufanya mazungumzo kwenye Almasi na Tanzanite,kazi hiii anze haraka na mapema"

"Naomba Barrick walipe hizo Tzs. Bil. 700 haraka kwasababu ninataka kuzitumia"

"Serikali ya Tanzania sasa tutaanza kufanya kazi moja kwa moja na Barrick"

"Barrick your true partner and your here to stay"

"Serikali hii ipo badala ya wananchi maskini,lazima watanzania tusimame pamoja"

Hotuba za Magufuli

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search