Thursday, 19 October 2017

BEKA FLAVOUR:KUNDI LA YAMOTO BAND LILISHAKUFA

Beka Flavour: Yamoto Band Imeshakufa Kila Msanii Anasimama Kivyake
Msanii wa Bongo Fleva, Beka Flavour amefunguka na kusema kuwa yeye kwa sasa hayupo tayari kurudi kwenye kundi la Yamoto Band na kudai ukweli ni kwamba kundi hili lilishakufa na kila msanii sasa anasimama kivyake.

Beka alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet bongo na kusema kuwa wakati wanaondoka kwenye kundi hilo hawakuwa na pesa zozote zile kwani enzi zao wakati wanafanya show mbalimbali walikuwa wanapewa fedha za matumizi tu na wao walipendekeza kwa uongozi fedha zinapopatikana wafanyiwe mambo kadhaa ikiwa pamoja na kujengewe nyumba.
"Mimi saizi ukisema nitoke kwenye uongozi wangu mpya nirudi Yamoto Band sidhani kama itawezekana unajua watu hawajui tu lile kundi ndiyo limeshakufa kwa sababu saizi kila msanii yupo na uongozi wake, sidhani kama wanaweza kukubaliana watoke walipo na kurudi kule" alisema Beka Flavour
Mbali na hilo msanii huyo aliweka wazi kuwa anafurahi kuona Aslay msanii ambaye alikuwa naye kwenye kundi moja na yeye saizi anakuwa ni kati ya wasanii wanaozungumziwa sana kwa kazi nzuri.
"Mimi nazidi kumuombea kwani mwenzangu saizi amekuwa ni kati ya wasanii ambao wanazungumziwa sana kutokana na kazi zake, lakini napenda kuwaambia Watanzania kuwa wasanii ambao tulikuwa tunaunda kundi la Yamoto Band Mungu alitupa kitu ndani yetu hivyo muda si mrefu mtakuja kuona  haya nayosema kwani kila mmoja ana upekee wake katika kazi zake" alisisitiza Beka 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search