Wednesday, 18 October 2017

CHADEMA: Lissu atoka ICU, anaweza kukaa...Kamera za CCTV karibu na aliposhambuliwa zimeondolewa
CHADEMA Tunaamini kabisa waliomdhuru Lissu wapo na wanajulikana. Tunaamini vyombo vya usalama wanawajua waliomshambulia Lissu.

Mh Lissu ni jirani wa Waziri,tuna taarifa kuwa ile cctv Camera iliyokuwepo eneo la tukio imeondolewa,imeondoolewa na nani?

Hatuna imani na Vyombo vya Dola vya ndani si kama havina uwezo, ni kwa sababu havina dhamira.

Nieleweke kwamba hatuvidharau Vyombo vyetu vya ndani, ila vinafanya kazi kwa mashinikizo, maelekezo ya viongozi wa Serikali."

Vyombo vyetu vya ndani havina dhamira ya kumtafuta Mhalifu kwa sababu tunapenda kuamini kwamba wanamjua mhalifu.

HALI YA TUNDU LISSU KWA SASA:

Tundu Lissu ametoka ICU wiki iliyopita na mashine zote zilizokuwa zikimsaidia zimetolewa. Hivi sasa anaweza kukaa.

Baada ya siku takribani 40 za matibabu, hatimaye TunduLissu ametolewa ICU na sasa anaweza kula na kukaa mwenyewe

Mh Lissu anaendelea vizuri hatumii tena mirija kula chakula,anakula chakula anachokitaka yeye"-

Lissu amepewa damu nyingi kuliko mgonjwa mwingine yeyote aliyewahi kuwa kwenye hospitali ya Nairobi kwa miaka 20 iliyopita.

Lissu anatarajiwa kumaliza awamu ya 2 ya matibabu ndani ya wiki 1 na atapelekwa nje ya Nairobi kwa ajili ya Rehabilitation

Tunajua kabisa uharamia huu kwa Lissu umetendwa na hao tunaowatuhumu na waliotenda wanajulikana na mfumo wa kutenda uliandaliwa

Limeanzia kwa Mh. Lissu na wengine tupo kwenye 'wanted list' huu utamaduni hatukuuzoea hivyo hatuwezi kulichukua kama jambo jepesi.

Nilikuwa nasita kutoa taarifa za mgonjwa kwa sababu ni haki ya mgonjwa na si jambo la chama.

Katika awamu ya tatu ya matibabu,tutaiachia familia nafasi kufanya maamuzi, tutasaidia pale tutakapohitajika kusaidia.

Kwa sasa anaendelea vyema na tutarajie kumsikia akizungumza kuanzia leo.

Pia tutaweka picha zake kwenye mitandao kwa mara ya kwanza tokea apigwe risasi. Kama kuna picha zozote zinazomuonesha Lissu akiwa hospitali hizo sio za kweli bali za kutengeneza.

Lissu ameshambuliwa imechukua masaa mawili polisi kufika kwenye eneo la tukio, Sisi tuamini akina nani waliotekeleza tukio hilo.

Ni kweli kuna mazungumzo yalifanyika kati ya Ofisi ya Bunge na Ofisi ya KUB kuhusu haki na stahiki za Tundu Lissu kama Mbunge

Ni ukweli usiopingika kuwa mgonjwa kutibiwa na Bunge ni haki yake ya kisheria. Haya mambo yana mihemko na hutulia baada ya muda.

Suala la Lissu lina hisia kali ndani yake. Msifikiri ni rahisi mtu akukosekose kukuua halafu aseme akulipie ukatibiwe.

Tunafahamu njama zinazopangwa, lakini hatutarudi nyuma. Tunaitwa viherehere kwa kumpigania Lissu lakini tunasema, hatutaukiri umauti

Kipaumbele chetu hakijawa fedha bali kumsaidia mgonjwa apone, mambo ya fedha tutayakuta tu.

Kama mtu ni haki yake asipoipata leo, iko kesho, iko keshokutwa. Hatuzungumzi kuhusu fedha, wakati utafika muafaka.

Michango ya Wabunge wote kwa kukatwa nusu ya posho zao za siku; kundi hili limechanga Tsh Milioni 43.

Wabunge wa CHADEMA wamechanga Tsh Mil 48, viongozi na wananchi Tsh Mil 24, wanachama mbalimbali Tsh Mil 90.

Misimamo ya Chama chetu haitayumbishwa na fedha pamoja na umasikini wetu. Tunajali utu, ulinzi na kila mtanzania apate haki ya kuishi.

GHARAMA ZA MATIBABU MPAKA SASA

Hadi tarehe 12 mwezi huu wa 10 gharama ya kila kitu kilichotumika kumtibu Lissu ni 18,352, 156 kwa Pesa za Kenya sawa na Mil 412,472,250 za Tanzania.

Tunawashuru wote kwa kutufuatilia LIVE hapa JF na kupata kile kilichosemwa na Kiongozi mkuu wa Upinzani Tanzania Freeman Mbowe kuhusu Yatokanayo na Afya ya Mwanasiasa mashuhuru zaidi Afrika Mashariki Tundu Antipas Lissu.

Mungu Awabariki Nyote.

Asanteni sana.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search