Thursday, 19 October 2017

Chadema Wamkataa Mkerugenzi wa Halmashauri ya Meru Kusimamia Uchaguzi

Chadema Wamkataa Mkerugenzi wa Halmashauri ya Meru Kusimamia Uchaguzi
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeweka wazi kwamba hakimuhitaji Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bw. Christopher Kazeri kuwa msimamizi wa uchaguzi mdogo kwa madai hawana imani naye pia hana sifa kwani anaweza kusababisha umwagikaji wa damu.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeweka wazi kwamba hakimuhitaji Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bwana Christopher Kazeri kuwa msimamizi wa uchaguzi mdogo kwa madai kwamba hawana imani naye pia hana sifa kwani anaweza kusababisha umwagikaji wa damu.
Akiitoa taarifa hiyo Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa amesema kwamba Mkurugenzi huyo alipoteza sifa za kusimamia uchaguzi tangu Juni, 24 walipokuwa kwenye uchaguzi wa vitongoji na vijiji  kwa kufoji matokeo katika vijiji kadhaa na kuwalazimisha wasimamizi wabadilishe namba kwenye fomu.
Golugwa amesema kwamba vitendo ambavyo Mkurugenzi huyo alivifanya anavitafsiri kama mambo ya kihuni kwani yalipelekea kugombanisha watu ambao ni ndugu hivyo hofu yao ni kwamba anaweza kusababisha umwagikaji damu katika uchaguzi mdogo wa marudiano Arumeru Mashariki.
"Tumeishauri Tume iweze kuwasiliana na mamlaka ya uteuzi kwamba hatumtaki ndg Kazeri awe msimamizi wa uchaguzi huu mdogo Arumeru Mashariki, kwanza aliingilia uchaguzi wa vitongoji na vijiji na kulazimisha kubadilishwa matokeo ambayo yalionyesha Chadema wameshinda, jambo ambalo lilileta ugombanishi kwa wagombea, na hata wagombea wa CCM walikataa matokeo kwa kukubali kwamba walishindwa na hata wasimamizi na askari waliokuwepo hapo walithibitisha kwamba Chadema walikuwa wameshindwa" Golugwa
Ameongeza  "Kama uchaguzi wa vitongoji Mkurugenzi ametumia mabavu na kufanya uhuni ambao tumeumbatanisha kwa Tume, kwenye uchaguzi huu wa madiwani si ataleta hata vifaru au kusababisha umwagaji wa damu? Kwa busara na hekima ya kawaida matendo aliyoyafanya Kazeri hayampi sifa ya kuwa msimamizi.
Hata hivyo Golugwa amefafanua na kusema kwamba wamewasilisha ushahidi wa wagombea wa CCM wakikataa kupokea ushindi huo wa vitongoji kwa madai kwamba hawawez kupokea ushindi wa  mtutu wa bunduki.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search