Thursday, 12 October 2017

Chanjo Dhidi ya Ugonjwa wa Ebola Yafanikiwa

Chanjo Dhidi ya Ugonjwa wa Ebola Yafanikiwa

Uchunguzi uliofanyiwa chanjo mbili tofauti za ugonjwa wa Ebola umebaini kuwa chanjo hizo zinaweza kumkinga mtu kutokana na virusi vya ugonjwa huo kwa takriban mwaka mmoja.
Utafiti huo uliochapiswa katika jarida la New England Journal of Medicine, ulifanyiwa nchini Liberia na kuwashirikisha wagonjwa 1,500
Wale waliopewa chanjo hiyo walifanikiwa kupata kinga yenye nguvu kwa karibu mwaka mmoja.
Chanjo ya Ebola yafanikiwa
Maziko salama yanusuru maisha Afrika Magharibi
Majaribio hayo yanaonyesha kuwa chanjo hizo zote zinaweza kutumiwa kuokoa maisha wakati wa majanga ya ugonjwa wa Ebola siku za usoni.
Ugonjwa wa Ebola uliwaua zaidi ya watu 11,000 nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea, wakati wa mlipuko wa ugonjwa huo mwaka 2014-2015

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search