Tuesday, 10 October 2017

CHUI MILIA ADIMU WAUA MHUDUMU WA MBUGA YA TAIFA YA WANYAMA

Mtunzaji wa wanyama katika mbuga ya taifa ya wanyama kusini mwa India ameshambuliwa na kuuawa na chui milia wawili, maafisa wanasema.

Mhudumu huyo wa miaka 40 aliuawa alipojaribu kuwaelekeza wanyama hao adimu sana kuingia kwenye kizimba chao Jumamosi usiku katika kituo cha wanyama cha Bannerghatta ndani ya mbuga hiyo.

Maafisa wanasema chui milia hao walimshambulia kwa sababu kizimba kimoja kati ya vizimba vinne kwenye mbuga hiyo hakikuwa kimefungwa vyema.

Chui hao hupata rangi yao nyeupe kutokana na kuwa na jeni mbili za rangi hiyo.

Jeni ya rangi nyeupe hujificha chui hao wakiwa na jeni ya rangi yao ya kawaida.

Mhudumu huyo alikuwa ameajiriwa katika mbuga hiyo wiki moja tu iliyopita.

Jamaa zake wenye hasira waliandamana kwenye mbuga hiyo Jumapili na wanataka walipwe fidia na wasimamizi wa mbuga hiyo ambao wanawatuhumu kwa utepetevu.

Mhudumu katika mbuga hiyo iliyo karibu na Bangalore alijeruhiwa vibaya na simba miaka miwili iliyopita.

Via>>BBC

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search