Wednesday, 18 October 2017

DROO YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA KWA NCHI ZA ULAYA HII HAPA

Droo ya kupata timu nne zitakazoungana na timu nyingine tisa kutoka ukanda wa UEFA kushiriki fainali za kombe la dunia mwakani nchini Urusi imefanyika hii leo jijini Zurich, Uswisi.
Droo hiyo imehusisha timu nane zilizoshika nafasi ya pili katika hatua ya makundi yao zikiwa na uwiano mzuri wa pointi.
Matokeo ya droo hiyo yanaonesha kuwa Ireland Kaskazini itaanzia nyumbani kucheza dhidi ya Uswisi wakati Ugiriki inakwenda ugenini kucheza dhidi ya Croatia.
Denmark atakuwa mwenyeji wa Jamhuri ya Ireland na Sweden dhidi ya mabingwa mara nne wa kombe la dunia Timu ya Taifa ya Italia.
Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa kati ya Novemba 9 na 11 wakati zile za marudiano zitachezwa kati ya Novemba 12 na 14.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search