Thursday, 5 October 2017

Familia ya Tundu Lissu wanaongea na Wanahabari
 1. Tunashukuru sisi kama wanafamila kwa kuitikia wito wetu

  Lute Simon Mughwai, kaka wa Tundu Lissu ni wakili na ofisi yangu ipo Arusha.
  Sababu za kuita hii press conferess ni kama zifuatazo;
  1. Kuwashukuru ninyi wanahabari kwa namna ambavyo mmendelea kutuhabarisha na kutoa habari kwa wananchi kwa umma juu ya maendeleo ya matibabu ya Mhe. Tundu
  2. Kwa niaba ya familia, naomba niweze kuwapa mrejesho juu ya hali ya Mhe. Tundu. Anaendelea vizuri ana imarika, amefanyiwa upasuaji mara kadhaa na sasa hivi yupo vizuri. Ameanza kula kwa njia ya kawaida na ameanza kuzungumza vizuri. Ndugu yetu ambaye ameenda kule mara ya mwisho juzi ameleta salamu kwamba yupo sawasawa na jana tumezungumza na mke wake
  3. Nilivyokwenda Nairobi tarehe 9, tulifanya kikao sisi wanafamilia, uongozi wa Chadema pamoja na uongozi wa chama cha wanasheria Tanganyika kwamba atakayekuwa natoa taarifa juu ya matibabu ya Tundu ni Mhe. Mbowe pekee. Yeye ndio atatoa taaarifa rasmi na wali si mwingine yeyote

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search