Thursday, 12 October 2017

HABARI KATIKA PICHA HAYA NDIO MAISHA YA WAKOREA KASKAZINI

Young children in a subway carriage
Haki miliki ya pichaNK NEWS
Image captionWanafunzi wakiwa safarini kurudi nyumbani wakitumia treni Pyongyang
Vitisho vya Donald Trump na Kim Jong-un, wote wawili wakitishia kuangamizana, vilipokuwa vinagonga vichwa vya habari duniani, maisha ya kawaida yalikuwa yanaendelea Korea Kaskazini.
Picha hizi zilizopigwa Septemba wakati wa ziara ya kundi la maafisa wa NK News zinaonesha watu wa kawaida wakiendelea na shughuli zao za kila siku.
Ni nadra sana kushuhudia athari za vikwazo ambavyo vimewekewa nchi hiyo na Marekani na jamii ya kimataifa au hata prapaganda kutoka Marekani.
Hapa chini, ni raia wa Korea Kaskazini wakiwa matembezini katika maporomoko ya maji ya Ullim karibu na mji wa bandarini wa Wonsan.
Wana chakula cha kutosha, bia na muziki, hakuna chochote cha kudokeza kwamba wanatishiwa na vitisho ambavyo vimekuwa vikitolewa na Marekani.
People picnicking in a partHaki miliki ya pichaNK NEWS
Wanafunzi hawa katika kambi ya watoto wanaonekana wakiwa wamevalia mavazi ya kimichezo ya kupendeza. Ukitazama kwa karibu utaona mavazi yao yana nembo za kampuni za nchi za Magharibi, Nike au Adidas.
Kuna uwezekano mkubwa kwamba ni ya kuigwa na kwamba watoto wenyewe hawana ufahamu wowote kuhusu kampuni hizo za mavazi kutoka nchi za Magharibi.
A group of young studentsHaki miliki ya pichaNK NEWS
Feri hii kubwa zamani ilitumiwa kuwasafirisha abiria kati ya mji wa Wonsan na mji wa bandarini wa Niigata nchini Japan.
Lakini kutokana na vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Korea Kaskazini mwaka 2006, huduma hiyo ya feri ilisitishwa.
Hii imefanya chombo hicho cha baharini kusalia bandarini Wonsan, lakini inaonekana kwamba wahudumu bado wapo.
Two women aboard a shipHaki miliki ya pichaNK NEWS
Chaza ni chakula maarufu sana katika miji ya pwani.
Wengi kawaida huuzwa nje badala ya kuliwa na wakazi.
Tangu kuwekwa kwa vikwazo vipya vya Umoja wa Mataifa ambavyo vilizuia nchi hiyo kuuza vyakula vya kutoka kwa wanyama wa baharini, sasa huenda wakaanza kuuzwa tena kwa wenyeji.
Two women grilling clamsHaki miliki ya pichaNK NEWS
Kwa muda mrefu, baiskeli zinazotumia umeme zilizokuwa zimeagizwa kutoka Japan au China zilikuwa zinapatikana katika mji mkuu wa Korea Kaskazini pekee.
Lakini sasa zimeanza kupatikana katika miji mingine midogo, ishara kwamba ukuaji wa uchumi unaanza kushuhudiwa nje ya Pyongyang.
Electric bicyclesHaki miliki ya pichaNK NEWS
Lakini uchukuzi bado umesalia kuwa wa kiwango cha msingi sana.
Miji mingi watu hutumia baiskeli.
Hapa mwanamume anaonekana akitumia kigari cha kuvutwa na ng'ombe kusafirisha kadibodi za kwenda kutumiwa tena kiwandani katika mji wa Hamhung.
Ox-drawn carriageHaki miliki ya pichaNK NEWS
Mwanamke aliye katikati kwenye picha hii ana mfuko wa plastiki wenye nembo ya duka la jumla kutoka Japan na China, duka la Miniso.
Kwa mujibu wa maafisa wa NK News, ambao walipiga picha hizi, Miniso walifungua duka lao la kwanza majira ya kuchipuza mjini Pyongyang.
Hatua hiyo iliwafanya duka la kwanza kutoka nje ya nchi kufungua maduka Pyongyang.
Hata hivyo, walibadilisha jina lao kutokana na vikwazo.
People in a public parkHaki miliki ya pichaNK NEWS
Ingawa maisha kwa kiwango kikubwa yanaonekana kuendelea kama kawaida, kuna dalili kwamba baadhi ya vikwazo vinaanza kuathiri maisha hapa.
Baadhi ya vituo vya mafuta vimefungwa na ukosefu wa umeme mara kwa mara umesababisha baadhi ya watu kujiwekea mitambo ya sola hata kwenye vyumba vyao vidogo, kama unavyoona kwenye jumba hili la makazi katika mji wa Kaesong, karibu na mpaka wa nchi hiyo upande wa kusini.
Apartment bloc with several solar panes attached to windowsHaki miliki ya pichaNK NEWS
Licha ya changamoto za kiuchumi, vita vya propaganda bado vinaendelea.
Kila mwaka, Siku ya Mwanzilishi wa Taifa husherehekea kwa dansi ya maelfu ya watu mji mkuu wa Pyongyang.
Mwanamke huyu anajiandaa kwa dansi hiyo.
North Korean dancerHaki miliki ya pichaNK NEWS
Kila wakati, taifa hilo huwa linatia akilini uwezekano wa kushambuliwa na adui kutoka nje.
Kuna mabando ya kushutumu Marekani pamoja na mabango yenye ujumbe wa kizalendo.
Waelekezi wa kitalii wa serikali huwapeleka wageni hadi kwenye Makumbusho ya Vita vya Ushindi na Ukombozi wa Taifa.
Licha ya wasiwasi ambao umekuwepo, watu bado wana sababu ya kutabasamu.
North Korean soldierHaki miliki ya pichaALAMY
Korea Kaskazini imesisitiza kwamba iko tayari kwa vita wakati wowote ule.
Hapa chini, ni 'mtego' wa kuzuia vifaru kupita.
Minara hii ya saruji ina vilipuzi na wakati wa vita hulipuliwa na kulaza minara hiyo barabarani kuzuia vifaru vya adui kupita.
Mitego hii sasa inaweza kuonekana ya zamani sana enzi hizi za vita vya makombora na silaha nyingine za nyuklia, hata hivyo, bado ni ukumbusho wa uwezekano wa kuzuka kwa vita wakati wowote.
A tank trap on a North Korean roadHaki miliki ya pichaNK NEWS
Vita dhidi ya Korea Kaskazini vinaweza kuwa vipi?
Picha zote zimetoka kwa NK News, jarida maalum kuhusu Korea Kaskazini. Wakati wa safari yoyote ile nchini humo, picha zinaweza tu kupigwa kwa idhini ya waelekezi wa safari wa serikali ambao wakati wowote huwa hapo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search