Friday, 6 October 2017

Hamisa Mobetto Amfungulia Kesi ya Madai Diamond Platnumz

Mwanamitindo Hamisa Hassan Mobetto amemfungulia kesi ya madai mzazi mwenzie, Msanii Naseeb Abdul @diamondplatnumz kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi pamoja na kutotoa fedha za matunzo ya mtoto wao, Abdul Naseeb Juma.
.
Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa @hamisamobetto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.
.
Katika wito huo Diamond anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.
.
Wakili Zulu akizungumza na Gazeti la Mwananchi, amesema mteja wao Hamisa Mobetto alimtumia Diamond notisi ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.
.
“Baada ya kuona kimya tulipeleka kes i katika Mahakama ya Kisutu upande wa watoto (The Juvenile Court Of Dar es Salaam) na leo(Alhamisi) tumepewa barua ya wito na tayari mwanasheria wa mwanamuziki huyo ameipokea,” amesema.
.
Shauri hilo linatarajiwa kutajwa ifikapo Oktoba 30, 2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search