Monday, 30 October 2017

Hatimaye FIFA wautambua rasmi ubingwa wa pili wa dunia wa Man United

Takribani baada ya miaka 18, hatimaye Manchester United wametambuliwa rasmi kuwa mabingwa wa dunia kwa ya pili kufuatia maamuzi mapya yaliyochukuliwa na FIFA.
Shirikisho hilo la soka duniani limesema kwamba limewatambua rasmi washindi wa kombe la Intercontinental Cup, ambalo lilikuwa linafanyika kuanzia mwaka 1960 mpaka 2004, mashindano yaliyokuwa yakishirikisha vilabu kutoka mabara tofauti duniani na kutoa bingwa wa dunia.
Mashindano haya mara nyingi yalikuwa yakishirikisha vilabu bingwa vya Ulaya na kutoka Amerika ya kusini – washindi wa wa Copa Libertadores.
Hata hivyo, mashindano haya yalikuwa na vurugu, kutokukubaliana kuhusu mfumo wa ufanyikaji wa mashindano na pia mataifa ya ulaya na vilabu vyake kutovutiwa na kushiriki. Liverpool, kwa mfano, walikataa kucheza dhidi ya Boca Juniors mnamo mwaka 1977 na 1978.
Vilabu vya Uingereza vina rekodi mbaya katika mashindano hayo, Celtic, Manchester United, Nottingham Forest, Liverpool (mara 2) na Aston Villa wakipoteza michezo ya fainali kabla ya United kuwafunga mabingwa wa Brazil mwaka 1999 – Palmeiras nchini Japan.
Red Devils pia wamefanikiwa kushinda kombe hili baada ya kubadilishwa jina na kuwa klabu bingwa ya dunia – mwaka 2008

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search