Tuesday, 17 October 2017

HAYA NDIO MAJIBU YA LUKAKU BAADA YA KUAMBIWA ALIFULIA DHIDI YA LIVERPOOL

Tangu ajiunge na klabu ya Manchester United mechi dhidi ya Liverpool ndio ilikuwa mechi ambayo Romelu Lukaku alibanwa sana na kwa mara ya kwanza mshambuliaji huyo alionekana akipotea uwanjani.
Klabu kubwa kama Manchester United hata ufanye mema mangapi lakini ukikosea mara moja tu baasi maneno yote mabaya yanaelekezwa kwako na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Lukaku.
Beki wa zamani wa Man United, Garry Neville aliongoza kundi la wachambuzi walioponda kiwango cha Romelu Lukaku huku mashabiki mbali mbali haswa haswa wasio wa United walianza kumshambulia mshambuliaji huyo wa Ubelgiji.
Lukaku ameyasikia maneno yote na amejibu kwamba hayambabaishi hata kidogo kwani wanaomsema wanaweza kwenda kuangalia alichofanya katika ligi kuu Uingereza msimu huu na kujua yeye ni nani.
Lukaku ameshangazwa na wanaomsema kupoteza nafasi aliyoipata kwa kusema kwamba kuna washambuliaji ligi kuu Uingereza ambao wanapata nafasi nyingi zaidi yake lakini wana magoli machache kuliko yeye.
“Kila mtu mara Rom hivi mara Rom vile na sielewi hata na kwanini, kila mtu atasema anachojisikia lakini ninachokifanya uwanjani kinaonekana” alimalizia Lukaku.
Manchester United walibanwa mbavu Jumamosi dhidi ya Liverpool huki wakipondwa kwa style yao ya kupaki basi ambayo waliitumia dhidi ya Liverpool.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search