Monday, 9 October 2017

HII NI HABARI MBAYA KWA MANCHESTER UNITED

Hakuna habari zenye uhakika kuhusu Paul Pogba, tetesi ni nyingi. Zipo habari kwamba amebakisha wiki mbili kurudi uwanjani huku wengine wakisema amebakisha mwezi mzima kurudi uwanjani. 
Lakini chanzo kimoja cha habari ambacho kinaaminika kimekuja na habari mbaya kuhusu Pogba, inasemekana kiungo huyo wa Ufaransa anaweza kukosa michezo mingi zaidi na asirejee hadi mwisho wa mwaka.
 
Habari hizo zinasema Paul Pogba atakuwepo nje ya uwanja hadi msimu wa sikukuu za Christmass na anaweza kuikosa Chelsea, Tottenham na pia anaweza kukosa mchezo wa Manchester Derby dhidi ya City.
 
Sasa wakati mashabiki wa United walishaanza kumsahau Paul Pogba kutokana na kiwango kizuri sana cha Mourruane Fellaini kumekuja taarifa kwamba Fellaini ni majeruhi na anaweza kukaa nje kwa miezi kadhaa.
 
Fellaini ameumia wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Ubelgiji huku kocha wake Roberto Martinez akisisitiza kwamba wana mashaka makubwa kuhusu majeraha ya Fellaini, hii leo taarifa kamili ya majeraha ya Fellaini inaweza toka lakini inatarajiwa kuwa mbaya sana kwa United.
 
Manchester United wamekuwa na msimu mzuri sana tangu msimu wa 2017/2018 kuanza lakini sasa jinamizi lililowaandama msimu uliopita la majeruhi linaonekana limerudi tena Old Traford kwa mara nyingine.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search