Friday, 6 October 2017

HITILAFU YA MITAMBO YA SONGAS NDIO CHANZO CHA KUKATIKA UMEME GHAFLA

Tanesco; Hitilafu ya Mitambo ya Songasi Chanzo cha Umeme Kukatika Ghafla Dar
Shirika la Umeme Tanzania limesema chanzo umeme kukatika ghafla umeme baadhi ya maeneo Dar es Salaam kumesababishwa  na hitilafu iliyotokea katika mitambo ya Songas.

Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji ameliambia gazeti hili kwa simu tukio lilitokea maeneo mbalimbali yakiwamo Ubungo na Mbezi.

"Tunaomba radhi wateja wetu kwa usumbufu uliojitokeza kwa kukosa huduma hii. Nawahakikishia mafundi wameshaanza kulifanyia kazi haitafika saa 5 usiku umeme utarudi katika hali yake.

Muhaji amesema tayari maeneo mengine ikiwamo Ubungo huduma imerudi katika hali yake ya kawaida baada ya mafundi kuanza kazi ya kurekebisha itailafu hiyo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search