Friday, 27 October 2017

Huyu Hapa Muigizaji wa Filamu Adai Kunyanyaswa Kijinsia na George Bush

Huyu Hapa Muigizaji wa Filamu Adai Kunyanyaswa Kijinsia na George Bush
Aliyekuwa rais wa Marekani George Bush ameomba msamaha kwa dhiki aliyosababisha baada ya muigizaji mmoja kumtuhumu wa kumnyanyasa kijinsia.
Heather Lind alisema kuwa rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 93 alimshika kutoka nyuma akiwa katika kiti chake cha magurudumo na kutamka ''mzaha mchafu'' wakati wakijiandaa kupiga picha.
Bi Lind alitoa madai hayo katika mtandao wa Instagram katika chapisho ambalo limefutwa.
Msemaji wa Bush alisema kuwa kisa hicho kilikuwa jaribio la ucheshi.
''Rais Bush alikuwa hawezi chini ya hali yoyote ile na kwa makusudi kumsababishia mtu dhiki na ameomba msamaha iwapo kitendo chake cha kuzua ucheshi kilimkosea bi Lind'', taarifa iliosambazwa kwa vyombo vya habari ilisema.

Bwana Bush alihudumu katika kipindi cha miaka mitano kutoka 1989 hadi 1993 na ni babake George W Bush ambaye alihudumu mihula miwili kati ya 2001 hadi 2009.
Mzee huyo anaugua ugonjwa wa kutetemeka

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search