Thursday, 12 October 2017

Jeshi la Polisi: Sheikh Ponda ajisalimishe Polisi ndani ya siku 3, vinginevyo hatokuwa salama  1. Kamanda Mambosasa akijibu swali la Mwandishi kutoka gazeti la Uhuru, kwanini Polisi walivamia Mkutano wa Shekhe Ponda jana, Kamanda amesema ni kwa makosa ya uchochezi na kuwa anatakiwa aripoti Polisi ndani ya siku tatu ili hatua stahiki zichukuliwe.

    Jana Jumatano Sheikh Ponda alitumia lugha ya uchochezi alipozungumza na waandishi wa habari na kutoa kejeli kwa Serikali.

    Amesema kukimbia kwake hakutasaidia chochote ni vyema ajitokeze kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu suala hilo.

    “Sheikh Ponda alikuwa anajua kwamba anafanya kosa kwa sababu aliwaambia waandishi waje saa nne yeye akawapigia baadhi waje kabla ya saa nne,’’ amesema.

    Kamanda Mambosasa amesema baada ya askari kufika eneo ambalo Sheikh Ponda alikutana na waandishi wa habari, waliwachukua waandishi na wafuasi wake kwa mahojiano. Baada mahojiano na Polisi kujiridhisha waliwaachia huru.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search