Saturday, 7 October 2017

Jukwaa la Katiba Kufanya Maandamano Nchi Nzima Octoba 30

Jukwaa la Katiba Yamuomba Magufuli Kupokea Maandamano ya Kufufua Mchakato wa Katiba

Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) limetangaza kufanya maandamano ya amani nchi nzima October 30, 2017 ili kurudisha hamasa kwa wananchi kushiriki kwenye michakato ya Demokrasia nchini.

Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda amesema kazi ya Jukwaa hilo ni kukuza hamasa ya wananchi kuweza kushiriki kwenye mchakato wa kuandika Katiba mpya.

Mwakagenda amesema kuwa kutokana na mkutano Mkuu wa dharula wa Jukata uliofanyika September 26, 2017 mjini Dodoma wameazimia kufanya maandamano nchi nzima.

”Maandamano yatafanyika October 30, 2017 ambapo kitaifa yatakuwa Dar es Salaam yakianzia Ofisi ya Jukata saa 4 asubuhi na yatahitimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.”

Aidha, amesema kuwa tayari wameshapeleka barua kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kwa ajilii ya kusudio la kufanya maandamano akiongeza pia kuwa wamemuandikia barua Rais Magufuli kumuomba apokee maandamano hayo ya amani.

Mwakagenda amesema, lengo la kumuandikia barua Rais ni kwa sababu Jukata inatambua jitihada zake katika kusimamia mambo yenye manufaa kwa Watanzania na vizazi vijavyo.

”Sababu nyingine ni kufikisha ujumbe wa haja ya kurejewa kwa mchakato wa Katiba mpya ya Tanzania ili tuukamilishe na kupata katiba mpya ya wananchi.”

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search