Thursday, 19 October 2017

KUHUSIANA NA KESI YA KANUMBA :-SHAHIDI TULIKUTA PANGA CHINI YA KITANDA CHA KANUMBA"

Leo Oktoba 19, 2017 mahakama kuu chini ya Jaji Sam Rumanyika imeanza kuisikiliza shauri la kesi ya jinai namba 125 ya mwaka 2012, Inayomkabili Msanii Elizabethi Michael ya kumua msanii mwenzie Steven Kanumba bila kukusudia mbapo leo upande wa jamhuri ulikuwa na Mashahidi 2 na shahidi namba moja alikuwa ni Mdogo wake Steven Kanumba Aliyejimabulisha kama Seth Bosco, lakini shahidi wa pili aliomba udhuru wa kutofika leo. 
Katika maelezo ya Shahidi Seth Bosco akiongozwa na wakili wa Jamhuri Faraja George ameieleza mahakama kuwa Kanumba ndiye aliye mfungulia mlango Lulu, na alipofika ndani baada ya muda kidogo yeye akiwa chumbani kwake alianza kusikia mvutano wa sauti ya Kanumba ikimwambia Lulu
"kwanini Unaongea na 'Boyfriend' wako mbele yangu?" Mabishano yalianzia kwenye korido, na baada ya kuingia chumbani zilianza kusikika kelele
Baada ya muda mfupi Lulu aliinita na kuniambia Kanumba ameanguka najaribu kumwagia maji naona haamki, nilipoingia chumbani nikweli nilikuta yuko chini akiwa ameegemea ukuta, nikamchukua nikamlaza chali na ndipo nilipoanza kumtafuta Daktari wake anayeitwa Paplas Kageiya, daktari alipofika alimfanyia 'Chek up' akasema ameshafariki, akashauri tumpeleke Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, niliendesha gari mpaka muhimbili, tulipofika muhimbili kwenye kitengo cha dharura walituambia tukatafute utaratibu wa kipolisi, wakati wao wanaandaa vibali vya kuruhusiwa apelekwe mochwari, Baada ya mahojiano ya Polisi katika kituo cha urafiki Ubungo, niliondoka na Askari kurudi nyumbani kwaajili ya uchunguzi, baada ya polisi kufika pale wakiwa chumbani wanaendelea na uchunguzi walikuta Panga chini ya kitanda" Alisema shahidi Seth Bosco

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search