Saturday, 7 October 2017

Maandamano ya Kupinga Kujitenga kwa Catalonia Kufanyika

Maandamano ya Kupinga Kujitenga kwa Catalonia Kufanyika

Wale wanaopinga juhudi za jimbo la Catalonia kujitenga leo wamepanga maandamano makubwa huko mjini Madrid wakisema Uhispania ni taifa moja na hawataki ligawanyike.
Sintofahamu hiyo imetokana na kufanyika kwa kura tata ya juzi ambapo Catalonia ilisema kura ndiyo ingeamua iwapo wajitenge .

Japo wanasema asilimia kubwa ya waliopiga kura waliunga mkono, bado hawajatangaza uhuru wao wala hakuna dola yoyote ya nje na ndani ya Uhispania inayoitambua.
Utawala wa serikali kuu ulitumia nguvu na mbinu tofauti tofauti kujaribu kuzuia kura hiyo .
Mzozo huo umesababisha wasiwasi mkubwa sio tu wa kisiasa bali pia wa kibiashara.
Mapema leo benki ya pili kuu Caixabank, imetangaza kuondoa makao yake makuu kutokana na wasiwaasi unaoendelea kuligubika eneo hilo

Shirika la fedha dunia ,IMF limesema mzozo huo unaharibu mazingira ya uwekezaji wa Catalonia.
Ni dhahiri pande zote mbili na hata jamii ya kimataifa zingependa kuona mzozo huo umesuluhishwa kwa majadiliano lakini bado hamna dalili zozote kwamba yatafanyika hivi karibuni.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search