Thursday, 19 October 2017

Mamake wa Mwanajeshi wa Marekani Amshtumu Trump kwa Kutokuwa na Huruma

Mamake wa Mwanajeshi wa Marekani Amshtumu Trump kwa Kutokuwa na Huruma
Rais wa Marekani Donald Trump amejipata mashakani kwa mara nyingine kuhusiana na kauli yake aliyoitoa kwa mjane wa mwanajeshi wa nchi hiyo aliyeuawa vitani nchini Niger.
Rais Trump amekana tuhuma kuwa alimwambia mjane wa mwanajeshi huyo kuwa mumewe alikuwa anajua kile alichoweka saini kwa kazi anayoijua hatma yake.
Mamake mwanajeshi huyo ambaye aliuawa wakati wa vita ameunga mkono madai ya bunge la Congress kwamba rais Trump hakuwa na huruma wakati wa mawasiliano ya simu na mkewe mwanawe marehemu.
Mbunge Federica Wilson alisema kuwa alimwambia Myeshia Johnson : Alijua alichokuwa ametia saini , ''lakini nadhani ni uchungu bila shaka''.

Bwana Trump alikuwa tayari amekosolewa kwa kutowasiliana na familia za wanajeshi waliouawa muda mfupi baada ya shambulio hilo la terehe 4 mwezi Oktoba.
Mamake sajenti Johnson , Cowanda Jones-Johnson aliunga mkono kauli ya mbunge Wilson kuhusu mazungumzo hayo ya simu.
Rais Trump hakumuheshimu mwanangu na mkewe pamoja nami na mume wangu , aliambia gazeti la The Washington post.

Kisa chengine kama hicho kilimlazimu rais Trump kumpatia fedha baba ya mwanajeshi mwengine aliyeuawa akiwa kazini , lakini habari kwamba hakulipa fedha hizo sasa zimejitokeza.
Alisema: Nitakuandikia hundi kutoka katika akaunti yangu binafsi ya $25,000, na nilidanganywa, baba huyo aliliambia gazeti la The Washington Post.
Ikulu ya Whitehouse iliambia gazeti hilo kwamba hundi hiyo ilitumwa na kwamba ilikuwa ishara ukarimu na uaminifu.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search