Thursday, 12 October 2017

Mavazi ya naibu gavana benki kuu Nigeria yazua mjadala mkali mitandaoni

Aisha Ahmad
Haki miliki ya pichaAISHA AHMAD/FACEBOOK
Image captionAisha Ahmad
Uteuzi wa mwanamke muislamu kuwa naibu wa gavana wa benki kuu nchini Nigeia, umezua mjadala mkali huku baadhi ya wale wenye misimamo mikali ya dini ya kislamu wakikosoa jinsi anavyo vaa.
Aisha Ahmad, 40, anatoka eneo la kaskazini mwa Nigeria, eneo ambapo wasichana wengi hupata masomo duni ikilinganishwa na sehemu za kusini mwa nchi.
Baada ya habari kuhusu kuteuliwa kwake kufichuka, mjadala uligeuka kutoka jinsi amehitimu na kuangazia mavazi yake.
Baadhi ya viongozi wa dini walio na wafuasi wengi mitandaoni walinukuu Koran, na kusisitiza kuwa wanawake ni lazima wavae kwa njia inayostahili
Picha zake zinamuonyesha akiwa amevaa nguo ya kawaida bila ya kujifunika kichwa chake
Lakini mwandishi mmoja nchini Nigeria Gimba Kakanda, ameiambia BBC kuwa, shutuma hizo zilivuka mipaka kwa kuwa eneo la kaskazini mwa nchi lina matatizo mengi ya kushughulikiwa 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search