Wednesday, 18 October 2017

Meneja wa Peacock Hoteli Akamatwa na Polisi kwa Kuhamasisha Ushoga

Image result for lazaro mambosasa


Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Polisi Dar es salaam Lazaro Benedict Mambosasa ambae ametangaza kukamatwa kwa Meneja wa Hoteli ya Peacock Dar es salaam.

“Tumewakamata Wahalifu wengine wa aina yake pale Peacock ambao wanahamasisha ushoga hapa nchini, Wahusika hao kuna raia wa South Africa, Waganda na Watanzania”

“Kwa Tanzania kuna sheria ya kuzuia watu wa jinsia moja kufanya tendo hilo, kwanza Meneja wa Peacock tumemkamata kwa ajili ya kumuhoji, alikua anafahamu ndio maana akatoa ukumbi lakini pia Wahusika hao warudi South Africa wakaendelee huko kama sheria zao zinaruhusu”


“Niliowakamata ni 12, raia wawili wa South Africa, Mganda mmoja na 9 ni Watanzania wenyeji ambao wametoka maeneo mbalimbali… niombe Watanzania kama walivyofanya pale Peacok waendelee kutuamini kwa kutoa taarifa ili tuweze kushughulika nao kwa wakati”

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search