Tuesday, 10 October 2017

MIFUPA YA BINADAMU YAKUTWA KWENYE BWAWA LILILOKAUKA LA TINDE - SHINYANGA


Habari zilizotufikia hivi punde kutoka kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga ni kwama mifupa inayodaiwa kuwa ni ya binadamu imekutwa katika bwawa la Tinde.

Mifupa iliyokutwa ni pamoja na taya yenye meno,mbavu,mfupa mmoja wa paja,mifupa mitatu ya mikono.

Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea leo jioni Jumatatu Oktoba 9,2017 wakati wananchi wakichimba kisima ndani ya bwawa hilo ambalo limekauka. 

“Kutokana na tatizo la ukame,wananchi walikuwa wanachimba kisima kwenye bwawa ambalo hivi sasa limekauka,wakati wanaendelea kuchimba ndiyo wakaona mifupa ya binadamu,hatujajua huyo mtu alifariki kwa njia gani,pengine alitumbukia kipindi bwawa lina maji ama alifukiwa na watu wasiojulikana”,kilieleza chanzo cha habari cha Malunde1 blog. 

"Mifupa iliyokutwa ni taya yenye meno,mbavu,mfupa mmoja wa paja,mifupa mitatu ya mikono",kimesema chanzo chetu cha habari.
Mkuu wa kituo cha polisi kituo cha Tinde pamoja na mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal (CCM) wamefika eneo la tukio. 

Taarifa zaidi tutawaletea hivi punde kupitia blog yako pendwa ya Malunde1 blog. 

Mwakilishi wa Malunde1 blog – Tinde,Said Nassoro ametutumia picha kutoka eneo la tukio,Tazama hapa chini
Mifupa inayodaiwa kuwa ni ya binadamu iliyokutwa kwenye bwawa la Tinde
Mifupa hiyo
Shimo ambamo kumekutwa mifupa
Wananchi wakishangaa
Wananchi wakishangaa mifupa hiyo
Mwananchi akishangaa mifupa hiyo
Mwananchi akikusanya mifupa hiyo
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal,mkuu wa kituo cha polisi Tinde na wananchi wakiwa eneo la tukio
Sehemu ya bwawa la Tinde likiwa limekauka

Bwawa likiwa limekauka

Picha zote na Said Nassor - Malunde1 blog - Tinde

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search