Monday, 30 October 2017

MOURINHO AKERWA NA MASHABIKI HAWA WA MAN UTD DHIDI YA LUKAKU

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amewatupia lawama mashabiki wa klabu ya Manchester United kwa kitendo cha kutokumuunga mkono mshambuliaji wao Romelo Lukaku.
Jose Mourinho anasema ameshangazwa sana na mapokezi ya Lukaku katika mchezo dhidi ya Tottenham na kusisitiza kwamba sio jambo la kiungwana kufanya hicho wanachofanya mashabiki wa United kwa sasa.
Mourinho anasema Romelu Lukaku anawapa Manchester United kila kitu alichonacho na anapambana kwa ajili ya timu hivyo haoni sababu ya mashabiki hao kumfanyia roho mbaya mchezaji huyo.
Mourinho amewataka mashabiki wa United kukumbuka mabao aliyowafungia klabu hiyo na kusema kwamba kwa anavyojitolea Mbelgiji huyo hakuna tofauti akifunga mabao na asipofunga.
Mourinho amesema anahisi mashabiki ambao wanamponda Romelu Lukaku kwa sasa watakuwa sio mashabiki wa Manchester United na labda watakuwa na klabu nyingine, Lukaku ana mechi 3 sasa za Epl hajafunga bao lakini ana mabao 7 katika mechi 10 alizoichezea United tangu ajiunge nao.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search