Tuesday, 31 October 2017

Mzazi Mwenzie na Joti Ampa Makavu Steve Nyerere

Mzazi Mwenzie na Joti Ampa Makavu Steve Nyerere 'Wewe  ni Mkubwaa Jielewe Ufupi Usikufanye Ukajiona Bado Mdogo'
Mwanamama aliyezaa na msanii wa vichekeshomaarufu kama Merisa Bushoke amemtolea povu Steve Nyerere baada ya kumpongeza Joti kwa kufanikisha kufunga ndoa .
Kupitia ukrasa wake wa instagram steve Nyerere alianza kwa kuandika hivi

 "Hii ni familia mpya ndugu yangu Joti ' hakuangalia ule usemi mama wa kambo si mtu mzuri ameangalia mapenzi na utu wa anayemuoa kwa watoto wake na familia yake si wamama wakambo wote wana roho mbaya apana, bali mazingira ya hiyo roho inawekwa na wewe baba kama huna misimamo ya familia yako kwa mwanamke mwenyewe mwenye kukupenda wewe  atapenda na watoto wako na familia yako. Joti jana ulilia ukumbini nikajiuliza kwanini ulilia  nikapewa jibu mtoto wako amepata mtoto bora  huo nao ni ujasiri  sana kuhakikisha  mama huyo mnayeingia naye  mkataba wa kidini anakuwa mama bora, tumekuwa watu wa kukalili unayezaa naye ndio mama bora  kumbe si kweli  Joti umetengua kauli Joti wewe ni shujaaaa,,,,," aliandika steve Nyerere

Baada ya posti hiyo ya Steve nyerere mwanamama huyo naye akajibu kupitia ukrasa wake wa Instagram ameandika hivi na kumtagi Steve Nyerere

"Naitaji kusema hivi huyu mtoto wangu na mm ndo niliemzaa haata mama awe chizi, tahila, mjinga ndo mama ake na hatokuja  kutokea yoyote  ukafananisha upendo wake  na mama yake  kwa hiyo sitaki  maneno na mtu  yeyote kama unataka kupongeza  kitu kizuri kilichoanyika  tumia maneno yasiyomuhusu mwanangu  nadhani umenielewa  na maana yako nini kuongea ulichoongea sijapenda wewe  ni mkubwaa jielewe ufupi usikufanye  ukajiona bado mdogo @stevenyerere2 @stevenyerere2

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search