Thursday, 5 October 2017

MZOGA WA KUKU ALIYEFUNGWA SANDA WAZUA GUMZO GEITA


Mzoga wa kuku aliyefungwa na sanda uliokutwa nje ya nyumba ya Emmanuel Kabodi.
Mama Mwenye nyumba Bi,Scolastica Nicodemo akizungumza na mmmoja wa viongozi wa dini waliofika kushuhudia mzoga huo
Wananchi wakishangaa
Viongozi wa dini wakiteketeza vitu pamoja na mzoga huo ambao umekutwa kwenye nyumba hiyo.
Wananchi wakiendela kushangaa tukio hilo

*****
Katika hali isiyo ya kawaida wananchi wa Mtaa wa 14 Kambarage Kata ya Buhalahala Wilaya na Mkoa wa Geita wamepigwa butwaa baada ya kukuta mzoga wa kuku ukiwa umevishwa sanda kwenye familia ya Emmanuel Kabodi.


Mama wa familia hiyo Bi Scolastica Nicodemo ameelezea kuwa wakati akifanya usafi aliona kuna kitu kimefungwa na shuka jeupe nyuma ya geti na alipojaribu kukiangalia aligundua ni sanda imefungwa kuku na ndipo walipofanya maamuzi ya kumwita mchungaji kuja kujionea.

Askofu wa kanisa la TMRC Mkoani Geita Stephano Saguda ameiasa jamii kuachana na masuala yanasosadikiwa kuwa ni ya kishirikina kwani vitendo hivyo havimpendezi Mungu na havikubaliki kwenye jamii ya watanzania .


Mjumbe wa Mtaa Huo Stephano Mayovu Matata amesema hii ni mara ya pili kutokea kwa tukio hilo kwani mara ya kwanza lilitokea tukio la kufukuliwa kwa mtoto na kwamba ni vyema kwa mtu ambaye anafanya vitendo hivyo kuachana navyo mara moja kwani wakimbaini mtu wa namna hiyo hawataweza kumvumilia.

Wananchi waliokuwa wamekusanyika katika eneo hilo wamesikitishwa na kitendo hicho kinachohusishwa na imani za kishirikina.

Mtaa wa 14 Kambarage umeendelea kukumbwa na vitendo vinavyosadikiwa ni vya imani za kishirikiana vya mara kwa mara na kusababisha hofu kubwa kwa watu ambao wanaishi maeneo hayo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search