Tuesday, 17 October 2017

Nape Nnauye: Watu Hawatakiwi Kuiogopa Serikali Yao Bali Serikali Inapaswa Kuogopa Watu Wake

Nape Nnauye: Watu Hawatakiwi Kuiogopa Serikali Yao Bali Serikali Inapaswa Kuogopa Watu Wake
Mbunge wa Mtama, Nape Moses Nnauye amefunguka na kusema kuwa watu hawapaswi kuogopa serikali yao bali serikali ndiyo inapaswa kuogopa watu wake.

Nape Nnauye amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ametumia maneno ya mwandishi wa vitabu maarufu kutoka nchini Uingereza Alan Moore ambaye mpaka sasa ameshaandika vitabu vingi vikiwepo Watchmen, V for Vendetta na From Hell.
Ujumbe huo alioweka Mbunge wa Mtama uliwekwa kwa lugha ya kiingereza " “People shouldn't be afraid of their government. Governments should be afraid of their people”  ukiwa na maana ya kuwa Watu hawapaswi kuogopa serikali yao bali Serikali inapaswa kuogopa watu wake.

Kufuatia ujumbe huo baadhi ya watu wameungana naye na kusema ndiyo ambavyo inapaswa kuwa huku wengine wakimpa changamoto kiongozi huyo
Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search