Thursday, 5 October 2017

RAIS MAGUFULI AZUNGUMZIA NDEGE YA BOMBADIER INAYSHIKILIWA CANADA

Rais John Pombe Magufuli amefunguka na kuzungumzia juu ya ndege za Tanzania sita zilizonunuliwa na serikali ikiwepo Bombardier Q 400-Dash ambayo inashikiliwa nchini Canada na kusema ndege hizo zitawasili nchini mwakani 2018.


Rais Magufuli amesema hayo alipokuwa kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT) ambao uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, Rais Magufuli amesisitiza kuwa Tanzania inakosa watalii wengi kutokana na kukosa ndege.


"Tumenunua ndege sita ndege mbili zimeshawasili Tanzania, lakini ndege zingine ikiwepo Bombardier zitawasilia mwakani 2018 mwanzoni. Tunafanya haya kwa ajili ya kutengeneza Tanzania mpya, nchi ambazo zina ndege zake idadi ya watalii wanaoingia kwenye nchi hiyo ni kubwa zaidi, nchi yetu ni ya pili kwa kuwa na vivutio vingi duniani lakini idadi ya watalii wanaoingia ni ndogo kutokana na kukosa ndege zetu" alisema Rais MagufuliSerikali ilikiri ndege mpya aina ya Bombardier Q-400 Dash 8 iliyonunuliwa na serikali ambayo ilipaswa kuingia nchini toka mwezi Julai lakini ikashindikana kufika kutokana na kudaiwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd iliyozuia ndege aina ya bombardier Q400-Dash 8 iliyonunuliwa na Tanzania nchini Canada.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search