Thursday, 19 October 2017

SAUTI YA LISSU AKIUNGURUMA: Awashukuru Watanzania kwa kumuombea

Sauti ya Mhe. Tundu Lissu akiwa Hospital Nairobi mapema leo hii.Kamanda Tundu Lissu amemshukuru Mungu kwakuwa bila yeye basi asingekuwa hai leo hii.

Rais huyo wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(Tanganyika Law Society - TLS) amewashukuru Watanzania waliomuombea na kumtembelea Hospitali. Pia amevishukuru vyama vya kitaaluma duniani kote.

Aidha Mheshimiwa Lissu amepokea jumbe za kuungwa mkono kutoka mataifa mbalimbali kama Marekani, Uingereza, Ujerumani, Autralia, Ubelgiji, na Kenya.

Madaktari na Wafanyakazi wote wa Hospitali ya Nairobi na wale wa Hospitali ya Mkoa wa DODOMA.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search