Thursday, 12 October 2017

Sehemu 10 ambapo wasichana hukumbwa na changamoto za kupata masomo

Sudan Kusini imetajwa kama mahala pabaya zaidi duniani katika masuala ya masomo kwa wasichana
Haki miliki ya pichaUNICEF
Image captionSudan Kusini imetajwa kama mahala pabaya zaidi duniani katika masuala ya masomo kwa wasichana
Mijadala kuhusu shule zilizo nchi tajiri uhusisha masuala tofauti, hasa ni masomo yapi yanayofaa kutiliwa maanani, nani yuafaa usaidizi zaidi na ni kipi kinahitaji fedha zaidi.
Lakini kwa familia zilizo katika nchi zinazoendelea, masuali kuhusu masomo yanaweza kuwa rahisi tu - je, kuna fursa yeyote ya kwenda shuleni?
Takwimu kutoka Umoja wa Mataifa inadadisi kuwa "hakujakuwa na hatua zozote" katika muongo mmoja kutatua ukosefu wa shule katika maeneo yaliyo maskini zaidi duniani.
Ripoti zaidi ilichunguza ubora wa elimu, na Umoja wa Mataifa ukasema kuwa matokeo yalikuwa ni ya kushangaza, kukiwa na zaidi ya watoto milioni mia sita walio shuleni lakini wanaopata masomo duni.
Nchini Niger, wanawake wanne kati ya watano wanasalia kutojua kusoma na kuandikaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNchini Niger, wanawake wanne kati ya watano wanasalia kutojua kusoma na kuandika
Maeneo yenyemigogoro
Kati ya nchi zote kumi, wengi wa wele wanaokosa fursa za kusoma ni wasichana.
Hizi ni nchi zilizo na migogoro, ambapo familia nyingi zinakubwa na hali ya umaskini, afya duni, lishe duni na kufurushwa makwao kutokana na vita na mizozo.
Wakimbizi wafurushwa kutoka makwao msimu huu nchini Sudan KusiniHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWakimbizi wafurushwa kutoka makwao msimu huu nchini Sudan Kusini
Wasichana wengi wadogo hufanya kazi badala ya kwenda shuleni. Na wengi huolewa wakiwa wachanga, na kuzima fursa yoyote ya kupata masomo.
Takwimu kutoka Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa wasichana wanauwezekano mara mbili zaidi wa kukosa masomo katika maeneo ya mizozo.
Wakimbizi nchini Chad: Migogoro imetatiza masomo ya mamilioni ya wanafunziHaki miliki ya pichaUNICEF
Image captionWakimbizi nchini Chad: Migogoro imetatiza masomo ya mamilioni ya wanafunzi
Viwango hivi huambatana na:
 • Idadi ya wasichana wasiokuwa na nafasi katika shule za msingi
 • Idadi ya wasichana wasiokuwa na nafasi katika shule za sekondari
 • Idadi ya wasichana wanaohitimu kutoka shule za msingi
 • Idadi ya wasichana wanaohitimu kutoka shule za sekondari
 • Miaka ambayo wasichana huanza kwenda shule
 • Idadi ya wanawake wasiojua kusoma na kuandika
 • Idadi ya walimu ikilinganishwa na wanafunzi
Katika baadhi ya nchi kama Syria, hakukuwa na takwimu za kubainisha ili kuwekwa katika orodha.
Hizi hapa sehemu 10 ambapo wasichana hupaa changamoto za kusoma:
 1. Sudan kusini: Zaidi ya robo tatu ya wasichana hawakufika shule ya msingi.
 2. Jamhuri ya Afrika ya Kati: kuna mwalimu mmoja kwa wanafunzi 80
 3. Niger: Asilimia 17 pekee ya wanawake kati ya miaka 15 na 24 wanaweza kusoma na kuandika
 4. Afghanistan: Kuna pengo kubwa la jinsia huku uwezekano wa wavulana kuwa shuleni kuliko wasichana ukiwa juu
 5. Chad: Masuala ya kijamii na uchumi inawazuia wasichana na wanawake kupata masomo
 6. Mali: Asilimia 38 pekee ya wasichana huweza kuhitimu kutoka shule za msingi.
 7. Guinea: wakati wastani wanaotumia wanawake zaidi ya miaka 25 katika masomo ni chini ya mwaka mmoja
 8. Burkina Faso: Asilimia 1 pekee ya wasichana humaliza masomo ya sekondari
 9. Liberia: Takriban theluthi mbili ya wanafunzi waliotimia umri wa kuenda shule za msingi hawaendi shuleni
 10. Ethiopia: Wasichana wawili kati ya watano wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18
Ukosefu wa walimu wa kutosha ni tatizo ambalo lilishuhudiwa kwenye nchi maskini.
Mwaka jana, Umoja wa Mataifa ulisema kuwa walimu milioni 69 zaidi, wanastahili kuajiriwa duniani kufikia mwaka wa 2030 ikiwa ahadi za kimataifa kuhusu masomo zitahitajika kutimizwa

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search