Tuesday, 10 October 2017

Shamsa Ford Apambana na Ndoa Yake Asema Hawezi Kumuacha Mumewe Kwa Sababu ya Amemsaliti

Shamsa Ford Apambana na Ndoa Yake Asema Hawezi Kumuacha Mumewe Kwa Sababu  ya Amemsaliti
Mwigizaji wa Filamu Shamsa Ford amesema hawezi kumuacha mumewe kwa sababu amemsaliti na mwanamke mwingine.

Shamsa amejilinganisha na Hillary Clinton aliyekuwa mke wa Rais wa 42 wa Marekani, Bill Clinton aliyewahi kuingia katika kashfa ya kuchepuka na Monica Lewnsinky.

Shamsa amesema anampenda mume wake kwa sababu anampenda na anajishusha kumuomba msamaha pale anampokosea.

“Nakupenda mume wangu halali wa ndoa aliyenipa mwenyezi Mungu. Sitoachana na wewe kwa ajili ya makelele ya wanadamu nitaachana na wewe kwa mapenzi ya mwenyezi Mungu,”

“Jamani sitokuja kumuacha mume wangu kwa ajili ya mwanamke hata siku moja labda afanye makubwa yasiyoeleweka kwenye jamii. ‘Amecheat’ Bili Clinton sembuse Rashid wangu? Alihoji mwigizaji huyo maarufu aliyecheza filamu ya Chausiku.

Katika siku za hivi karibuni mwigizaji huyo amekuwa akirusha vijembe kwa mwanamke anayedai kumtumia ujumbe mume wake na kutoa taarifa kwa wanahabari ili wamwandike vibaya.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search