Thursday, 19 October 2017

Siku tatu baada ya Mwigamba kujivua uongozi ACT Wazalendo ili aweze kuhoji uongozi, leo yeye na wenzake wajiunga CCM

Baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi Taifa ya Chama cha ACT Wazalendo kusema kuwa amejivua cheo hicho katika chama chake na kubaki kama mwanachama wa kawaida ili aweze kuhoji uongozi wa chama chake (ACT Wazalendo) ambao unaonekana haufanyi mambo sawa.

Leo hii Samson Mwigamba na wenzake wamejivua uwanachama na kujiunga na chama cha Mapinduzi (CCM)Wenzake Samson Mwigamba walijiunga na CCM ni pamoja na:-
Afisa wa Sheria wa chama cha ACT Wazalendo Taifa, Mwantum Mgonja, Katibu wa mkoa wa Singida wa ACT Wazalendo, Mchungaji Lotti.

Pia yupo Katibu wa ACT Wazalendo mkoa wa Arusha - Mchungaji Willison Laizar

Pia Mwenyekiti wa ACT Wazalendo mkoa wa Singida - Wilfred Kitundu

Emmanuel Kitundu - Afisa tawala ACT Wazalendo Makao makuu

Nakamia John - Mwenyekiti ACT Wazalendo jimbo la Singida Mjini

Peter Lucas Mwambuja - Mwekahazina wa chama Taifa

Danny Ollotu - Alikuwa Katibu wa chama mkoa wa Arusha kabla ya Willison pia ni Meneja Kampeni za Urais 2015.

Mwigamba amesema wamefikia uamuzi huo kwa sababu zifuatazo:-
Mwigamba "Tumefikia uwamuzi wa kujivua uwanachama wa ACT wazalendo baada ya kuamini na kushuhudia kuwa uongozi wa sasa wa chama hiki unachepuka kwa kasi mno nje ya misingi ya chama na sasa chama kimebaki kuwa jahazi ambalo tanga lake limechanika na likakosa muelekeo na hivyo kubaki kuyumbishwa kila upande kutegemea na mawimbi ya bahari yanayolipiha jahazi hilo."

"Hata hivyo sisi ni wana siasa na uwanja wa wanasiasa ni chama cha siasa, kwa mwanasiasa chama cha siasa ni kama timu cha mpira kwa mchezaji. Huwezi kuwa mchezaji mahiri na huna timu halafu unajiita ni mchezaji wa kulipwa"

Tumetafakari na kuchanganua vyama vilivyopo vya siasa na baada ya tafakari yetu tumeamua kujiunga na CCM kwa sababu zifatazo;

  1. CCM ya sasa ndio chama kinacho-act kwa karibu iktikadi, falsafa na sera za ACT Wazalendo ambazo mimi na wenzangu tulishiriki kuziasisi. Wakati tunanazisha chama cha ACT tulisema Chama kinalenga kuhuisha misingi iliyoimarisha taifa na sera zake zitalenga kufufua uzalendo, upendo, umoja, na mshikamano wa watanzania wote bila kujali dini jinsia na ufuasi wa chama cha siasa
  2. Kujiunga katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Tulifikia mahali watanzania hatuamini tena kuwa mafanikio hutokana na kujitegemea na bidii katika kazi, tuligeuka kuwa taifa la watu wanaishi kiujanja ujanja na wezi wa mali za umma wakisifiwa na kuchekewa. ACT tulisema hali hii haikubaliki na lazima turudi katika misingi. Serikali na rais Magufuli ipo katika vita kali dhidi ya rushwa na ufisadi na kila mtu anajua. Na leo nchi yetu ndio kinara wa mapambano zidi ya rushwa, lakini sasa upinzani ambao ndio uliasisi vita dhidi ya ufisadi umegeuka kuwa ndio watetezi wa mfumo wa kinyonyaji ulioutesa nchi kwa miaka mingi. Sisi tumeamua kujitenga na aina hii ya upinzani
  3. Kujitenga na upinzani unaokerwa na mafanikio ya serikali. Tangu wanachama wenzetu Prof. Kitila Mkumbo na mama Anna Mghwira, walipoteuliwa kufanya kazi katika utumishi wa umma katika serikali ya rais Magufuli. Uteuzi ambao kama chama tuliunga mkono na tamko lilitolewa na kiongozi wa chama kwa niaba ya chama kuunga mkono na kumpongeza rais kwa uteuzi huo. Lakini viongozi wetu wamekuwa wakikerwa na kutishwa na utekeklezaji wa majukumu yao, hususani pale wanapoelezea mafaniko ya serikali ambayo wao ni sehemu yake. Kwa sababu hii kumejengeka tabia ndani ya chama ya kuwazodoa na hata kuwatishia kuwavua uwanachama wao wanachama wenzetu ambao kimsingi walifanya kazi kubwa katika kukijenga na kuanzisha chama hiki. Hakuna aiyejua kazi walizofanya waasisi hawa, kama ningeulizwa muasisi namba moja ningemyaja Prof. Ktila Mkumbo na si Zitto Kabwe
Sasa tunahoji kama inakuwa kero kusikia mafanikio mbalimbali ya serikali, treni ya umeme, wakala wa barabara vijijini, mradi wa umeme wa stiegler's gorge, kusambazwa kwa maji vijijini, Kwanini tuliruhusu mama Anna Mghwira kumkabidhi rais Magufuli ilani yetu?

Kwanini kiongozi wetu, kiongozi wa chama alikataa kutoka bungeni siku ya hotuba ya rais ya uzinduzi wa bunge? Na alipoulizwa baadae akasema lazima amuunge mkono rais kwa kuwa aliyo yazungumza 60% yapo kwenye ilani ya uchaguzi ya ACT. Ni kitu gani kimebadilika leo?

Pia Mwigamba amesema matatizo ya ndani ya ACT wazalendo yameeanza baada ya uchaguzi mkuu wa chama, wa 28 March 2015. Baada ya uchaguzi ule ndipo tukapokea wanachama wafuasi wa watu, waliingia kwa wingi. Ndipo wanachama waliokuwepo waliokuwa wafuasi wa misingi wakaanza kuonekana hawana thamani na hawajui siasa.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search