Monday, 9 October 2017

TUNDU LISSU KUFANYIWA UPASUAJI WA 15

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amefanywa upasuaji mara 14 na ataendelea kufanyiwa upasuaji mwingine wa  15  ndani ya wiki mbili zijazo.

Mbowe amesema hayo jana kwenye mazishi ya marehemu Philip Gekul, baba mzazi wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata ya Dareda.

Alisema hali ya Lissu inaendelea kuimarika lakini aliumizwa sana kama walivyokuwa wanaeleza mara zote lakini na jambo la kumshukuru Mungu kwamba ameendelea kuimarika.

"Ameendelea kupata afya, akili zake ni timamu, madaktari kule wanafanya kazi kubwa kwelikweli kuendelea kumuudumia na ni matumaini yetu kuwa baada ya muda Mungu atamrejesha katika wajibu wake wa kulitumikia Taifa,"

Mbowe alizungumza hayo baada ya kueleza kuwa alitokea Nairobi kuangalia afya ya mbunge huyo ambaye alipigwa risasi Septemba 7 mwaka huu akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search