Wednesday, 11 October 2017

Zaidi ya Walimu 20,000 Waliofeli Mtihani Iliyotakiwa Kufanywa na Wanafunzi Wao Kufutwa

Zaidi ya Walimu 20,000 Waliofeli Mtihani Iliyotakiwa Kufanywa na  Wanafunzi Wao Kufutwa
Mamlaka katika jimbo lililo kaskazini mwa Nigeria la Kaduna zinasema kuwa zaidi ya walimu 20,000 wa shule za msingi watafutwa baada ya wao kufeli mtihani unaotahili kufanywa na wanafunzi wao.
Hii inafuatia madai kuwa nyingi ya shule za msingi na sekondari nchini Nigeria huzalisha wanafunzi wasiohitimu vyema.
Gavana wa jimbo la Kaduna el-Rufai alisema kuwa walimu waliohitimu wataajiriwa kuchukua mahala pa wale watakaofutwa.
Haijulikani hatua hii itachukuliwa lini.
Marufuku nguo za kubana chuoni Lagos
Wasichana waonywa dhidi ya kupotoshwa na mitandao ya kijamii Nigeria
Afisa mmoja wa cheo cha juu katika jimbo la Kaduna aliambia BBC kuwa mitihani zaidi itatolewa siku zinazokuja kwa walimu wa sekondani.
Wadadisi wanasema kuwa idadi hiyo ni ishara ya viwango duni vya elimu nchini Nigeria ambapo inadaiwa kuwa walimu huajiriwa kwa misingi ya kisiasa.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search