Thursday, 9 November 2017

AFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA BAADA YA KUPATIKANA NA HATIA YA KUMBAKA MTOTO WA KIKE WA DARASA LA PILI

Image result for MAHAKAMA
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imemuhukumu Lazaro Peter Ngomalala (50)  Mkazi wa Kijiji cha Simbwesa Wilaya ya Tanganyika kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka tisa jina limehifadhiwa mwanafunzi wa darasa la pili wa shule ya msingi Simbwesa.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashitaka akiwemo mwanafunzi huyo aliyebakwa uliotplewa Mahakani .

Kabla ya kutoa hukumu hiyo Hakimu Ntengwa alisema mtu yeyote anayefanya kitendo kama alichofanyiwa mtoto huyo anakuwa amefanya kosa kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 130 kifungo kidogo cha kwanza na cha pili na na kifungu cha sheria namba 131 kifungu kidogo cha tatu cha kanuni ya adhabu .

Alieleza kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka akiwemo mtoto mwenyewe na mtoto mwenzake ambaye alishuhudia tukio hilo,  mahakama pasipo shaka yoyote imemwona mshtakiwa Lazaro Ngomalala kuwa anayo hatia .

Ntengwa alisema miongoni mwa ushahidi wa sababu zilizoifanya mahakama imtie mshtakiwa hatiani ni ushahidi uliotolewa mahakamani na mtoto aliyebakwa na mtoto mwenzake mwenye umri wa miaka saba licha ya kuwa na umri mdogo walitoa ushahidi kwa ufasaha mkubwa juu ya tukio hilo.

Pia Mahakama ilijiridhisha na ushahidi uliotolewa na muuguzi wa zahanati ya Simbesa aliyemfanyia uchunguzi na kubaini kuwa mtoto huyo alikuwa amebakwa hali ambayo ilimlazimu muuguzi huyo amwanzishie dawa ya kuzuia maambukizi ya VVU.

Kabla ya kusomewa hukumu hiyo,  hakimu Ntengwa alitoa nafasi kwa mtuhumiwa Lazaro kama anayo sababu ya msingi ya kuishawishi mahakama iweze kumpunguzia adhabu hivyo mshitakiwa aliiomba Mahakama imwachie huru kwa kile alichodai kuwa yeye hakutenda kos hilo bali amesingiziwa na mama mzazi wa mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimdai fedha alizokuwa anamdai baada ya kumkopesha.

Baada ya utetezi huo wa mshtakiwa hakimu Chiganga Ntengwa alisema kutokana na mshitakiwa kupatikana  na hatia ya kifungu cha sheria namba 131 kifungu kidogo cha cha tatu kinachoeleza mtu yoyote atakayembaka mtoto mwenye umri wa chini ya miaka kumi adhabu yake ni kifungo cha maisha jela.

Hivyo kutokana na mshtakiwa Lazaro Ngomalala kupatikana na kosa hilo mahakama imemuhumu kuanzia jana kutumkia jela kifungo cha maisha jela.

Awali kwenye kesi hiyo Wakili wa Serikali Fravian Shiyo alidai mahakamani hapo kuwa Lazaro alitenda kosa hilo hapo Oktoba 12 mwaka 2016  majira ya saa nne asubuhi kijiji katika Jijiji cha Simbwesa.

Ilidaiwa kuwa siku hiyo ya tukio mshitakiwa alikuta mtoto aliyemtenda kitendo hicho akiwa na mtoto mwenzake wakiwa wanacheza jirani na nyumba yao ndipo alipowadanganya wamfuate nyumbani kwake ili akawapatie fedha za kununulia biscuit na soda. .
Shiyo alieleza kuwa wakati wakiwa wanaelekea nyumbani kwa mshitakiwa walipofika kwenye eneo la tanki la maji Lazaro alimvuta kwa nguvu mtoto huyo na kuanza kumbaka licha ya mtoto huyo kupiga kelele lakini hakuweza kumwachia mpaka alipo maliza haja yake .

Mwanasheria aliiambia mahakama baada ya kufanyiwa kitendo hicho mtoto huyo aliyebakwa alikwenda kutoa taarifa kwa wazazi wake huku akiwa analia na baada ya kutoa taarifa kwa wazazi wake mtuhumiwa alikamatwa na askari wa mgambo wa kijiji cha Simbwesa na kisha alifikishwa katika kituo cha polisi.

Na Walter Mguluchuma- Malunde1 blog Katavi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search