Monday, 13 November 2017

AJALI KATI YA LORI NA NOAH YAUAWA WATU WATANO MKOANI KILIMANJARO

 Habari kutoka Wilayani Hai ,mkoani Kilimanjaro watu watano wamepoteza maisha na wengine wanne wakijeruhiwa baada ya lori kugongana uso kwa uso na Noah maeneo ya kikavu kwa Sadala.

Daktari wa zamu hospitali ya wilaya ya Hai,Agness Temba amesema amepokea miili ya watu wa tano.

Amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Hai, na majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi.
Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search