Thursday, 16 November 2017

ALIYEKUWA MUME WA IRENE UWOYA NDIKUMANA HAMAD KATAUT AFARIKI DUNIA


Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Timu ya Soka ya Rayon Sports nchini Rwanda, Hamad Ndikumana Katauti amefariki dunia ghafla leo hii.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Rayon Sports Gakwaya Olivier, amesema kifo cha Ndikumana kilisababishwa na ugonjwa wa moyo.

“Alisikia maumivu makali kifuani akaomba soda ya baridi wakamletea na alipomaliza kunywa tu kidogo akatapika na akaishiwa pumzi na ndipo akakata kauli,” alisema Olivier na kuongeza kwamba bado wanasubiri uchunguzi wa madaktari.

Ndikumana ambaye amewahi kucheza soka Tanzania akiwa na klabu ya Stand United, amewahi kuwa mume wa muigizaji Irene Uwoya na wana mtoto mmoja.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search