Thursday, 23 November 2017

AMUUA MKEWE KWA KUKATAA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA

Migogoro ya kiyumbani ndio yenye visa vingi vilivyoripotiwa dhidi ya wanawake nchini India kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.
Image captionMigogoro ya kiyumbani ndio yenye visa vingi vilivyoripotiwa dhidi ya wanawake nchini India kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa mwanamume mmoja katika jimbo la kaskazini mwa India la Haryana amemuua mkewe baada ya kukataa kushiriki naye tendo la ndoa.
Sanjiv Kumar mwenye umri wa miaka 35 alidaiwa kumyonga mkewe ,Suman wakati wa vita siku ya Jumanne.
Mwanamume huyo alikiri kutekeleza kitendo hicho baada ya kukamatwa , afisa wa polisi Ramesh Jaglan aliambia BBC.
Migogoro ya kiyumbani ndio yenye visa vingi vilivyoripotiwa dhidi ya wanawake nchini India kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.
''Alikuwa akikataa kufanya ngono kwa muda .Siku ya Jumanne alikataa tena, hatua iliomuudhi na kuamua kumnyonga.Tumemkamata'', bwana Jaglan aliambia BBC.
Wanandoa hao walikuwa wameoana kwa zaidi ya muongo mmoja. Wana watoto wawili

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search