Friday, 17 November 2017

BABA YAKE KANUMBA-HUKUMU ILIYOTOLEWA DHIDI YA LULU NI KAMA YA MWIZI WA KUKU


Saa chache baada ya mahakama kumhukumu Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwenda jela miaka miwili kutokana na kifo cha Steven Kanumba,Baba wa marehemu Steven Kanumba mzee Charles Kanumba ameibuka na kueleza kuwa hukumu hiyo haijamfurahisha akifananisha hukumu hiyo kuwa kama hukumu ya mwizi wa kuku. 

Akizungumza na Malunde1 blog,Mzee Kanumba anayeishi Mjini Shinyanga alisema hukumu hajaridhika nayo kwani hukumu ya miaka miwili ni danganya toto kwa ndugu na wazazi hivyo ni bora wamuachie huru ijulikane moja.

Alisema hukumu ya kwenda jela miaka miwili haitoshi kwani anaifananisha na hukumu inayotolewa kwa wale wanaoiba kuku siyo kwa yule aliyesababisha mtu kupoteza maisha hata kama aliua bila kukusudia.

“Nimeipokea hukumu iliyotolewa na mahakama..lakini hivi sasa sina cha kusema kwani tangu kesi ilipoanza ilionekana kutotendeka haki mfano mtuhumiwa kuendelea kuwepo 

Alisema kabla ya kutolewa hukumu hiyo tarehe 13 Novemba mwaka huu aliiota ndotoni kuhusu hukumu ya kesi hiyo na kuieleza familia yake kuwa yuko mahakamani na hakimu akiwepo Lulu na mama yake mzazi na hukumu ilivyotolewa jana ni vile vile kama alivyooteshwa lakini hajawahi kuwaona ana kwa ana watu hao.

“Mimi nasema kuwa sijawahi kumuona ana kwa ana huyo binti anayeitwa Lulu na wala sijawahi kusikia sauti yake kwenye simu hata mama yake mzazi simjui bali watu hawa huwa ninawaona kupitia magazetini au kwenye televisheni tu basi”,alisema Mzee Kanumba.

Mzee Kanumba alisema marehemu Steven Kanumba alikuwa mwanaye wa sita na kifo chake kimeacha kubwa.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search