Friday, 10 November 2017

BASI LINALOJIENDESHA LENYEWE LAPATA AJALI SIKU YA KWANZA KUTOA HUDUMA

Basi linalojiendsha huko Las Vegas lilihusika kwenye ajali wakati wa siku yake ya huduma.

Gari hilo lililokuwa limewabeba abiria kadha liligongwa na lori lililkuwa katika mwendo wa chini.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa wakati wa ajali hiyo ambayo maafisa wanaema ilitokana na hitilafu ya dereva wa lori.

Basi hilo ndilo la kwanza la aina yake kutumiwa kwenye barabara za umma.

Ajali hiyo ilitokea siku moja baada ya Waymo - inayomilikiwa na kampuni ya Google, Alphabet, kutangaza kuwa inazindua teksi zinazojiendesha huko Phoenix, Arizona.

Basi hilo linawabeba hadi wau 15 na lina kasi ya hadi kilomita 45 kwa saa lakini kawaida mwendo wake ni kilomita 25 kwa saa.

Msemaji wa mji wa Las Vegas aliiambia BBC kuwa ajali hiyo ilkuwa ni kidogo na kwamba basi hilo litarudi barabarani Alhamisi baada ya majaribio ya kawaida.

Lori la mizigo lilikuwa likitoka kupakia mizigo.

"Basi likafanya kile linastahili kufanya na kusimama. Kwa bahati mbaya dereva wa lori hakusimama, alisema afisa wa mawasiliano Jace Radke.

Ajali za magari yanayojiendesha zimeripotwa awali, lakini karibu ajali hizo zote zimesababishwa na makosa ya wanadamu.

Chanzo- BBC

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search