Wednesday, 29 November 2017

BIBI WA MIAKA 73 ADAI TALAKA


Mwanamke ambaye yupo kwenye ndoa kwa miaka 55, nchini Kenya amefungua kesi mahakamani kuomba mumewe ampe talaka kwa madai kuwa hamjali, na anamthamini zaidi mke mdogo.

Mwalimu huyo mstaafu, Marcella Mukami Kinyugo (73), anaiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kangema, isitishe ndoa yake na Peter Kinyugo (76) iliyofungwa Septemba 16, 1962 katika Kanisa Katoliki Kiriaini.

Bibi huyo mkazi wa mjini Kiria-ini, Mathioya, kwenye kaunti ya Murang’a, pia aliomba apewe nusu ya mali za familia yao na pia mumewe alazimishwe kulipa gharama za kesi.

 Katika kesi hiyo bibi huyo aliwakilishwa na Margret Nyangati kutoka kampuni ya mawakili ya Muchoki Kang’ata.

Aliieleza Mahakama kuwa, waliishi maisha ya furaha ya mume na mke tangu walipofunga ndoa, lakini miaka sita iliyopita hali ilibadilika wakati mumewe alipoacha kutimiza majukumu yake kama mume.

Mume wa bibi huyo ni mwalimu mstaafu na Chifu. Mukami alidai mahakamani kuwa matatizo yalianza baada ya Kinyugo kukaa kwa mke mdogo kwa wiki kadhaa bila kwenda kwake, na kwamba, yeye na mke mwenzake wanaishi kwenye eneo moja. Kwa mujibu wa bibi huyo, wakati mumewe anafanya hivyo, hawakuwa na ugomvi.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search