Wednesday, 8 November 2017

BOMU LAUA WANAFUNZI SITA NA KUJERUHI WENGINE ISHIRINI NA TANO MKOANI KAGERA

Wanafunzi sita wa shule ya msingi Kihinga mkoani Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania wamefariki dunia na wengine zaidi ya 25 wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu wakicheza.

Kamanda wa polisi wa mkoa, Augustine Orom huo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wananchi wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.

Kwa mujibu wa  mganga mkuu hospitali ya Rurenge,Dokta Mariagoreth Fredrick amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu. 

"Tulionao hali ya sio nzuri. Wengine wameumia matumbo, wengine wamechanika bandama, wengine wamevunjika miguu, wengine vichwa vimepata majeraha, wengine wameumia macho." Dokta Mariagoreth ameiambia BBC. 

Inaelezwa kwamba kabla ya kulipukiwa na kifaa hicho kinachoarifiwa kuwa ni bomu, wanafunzi hao walikuwa wanakichezea. 

Wataalam wa afya wakitoa huduma kwa majeruhi
Wataalam wa afya wakitoa huduma kwa majeruhi
Wataalam wa afya wakitoa huduma kwa majeruhi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search