Thursday, 16 November 2017

BWANA HARUSI APIGWA RISASI SEHEMU ZA SIRI


Ufyatuaji wa risasi kusherehekea swala fulani katika eneo la mashiriki ya kati ni kitu cha kawaidaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUfyatuaji wa risasi kusherehekea swala fulani katika eneo la mashiriki ya kati ni kitu cha kawaida
Bwana harusi moja nchini Misri anejaruhuwa vibaya baada kupigwa na risasi iliokuwa imefyatuliwa ili kusherehekea harusi yake.
Bwana harusi huyo alipata majeraha mabaya katika sehemu yake ya siri , nyongani na mkononi na anatibiwa hospitalini.
Osman al-Alsaied mwenye umri wa miaka 28 alikuwa akisherehekea usiku wake wa mwisho akiwa kapera wakati silaha hiyo ilipofyutuliwa upande wake badala ya hewani.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa bunduki hiyo ilifyatuliwa kiuzembe na mwananume mwenye umri wa miaka 26.
Wanasema kuwa alitoroka muda mfupi baadaye baada ya kisa hicho lakini akakamatwa na sasa anahojiwa.
Ripoti za kisa hicho zimechochea hisia kali katika mtandao wa kijamii huku wengi wakitaka sherehe ya kufyatua risasi hewani kusitishwa.
Sherehe za harusi nchini Misri hupendwa sanaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSherehe za harusi nchini Misri hupendwa sana
Iwapo unafyatua risasi wakati unasherehekea furaha yako je itakuwaje wakati unapokasirika, ujumbe mmoja wa Twitter uliuliza.
Kulikuwa na kisa kama hicho katika harusi nchini Misri mwezi uliopita kulingana na mtandao wa Stepfeed.
Katika kisa hicho bwana harusi alifanyiwa upasuaji na matibabu baada ya risasi kumpiga katika nyonga yake

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search